The House of Favourite Newspapers

Aina 3 za Sickle Cell Unazopaswa Kuzijua-2

0

MAKALA: NA MWANDISHI WETU| UWAZI:  Tabibu

Wiki iliyopita nilianza kuelezea dalili za ugonjwa wa sickle cell, leo nitaendelea, ungana nami.

DALILI ZA UGONJWA

Mtu mwenye sickle cell anaweza kusikia kupooza mwili, maumivu sehemu za kifua, miguu na tumboni na anaweza kuambukizwa kirahisi magonjwa.

Aidha, mgonjwa anaweza kupata vidonda vidogovidogo kwenye miguu ambavyo hataweza kujua vimetokana na nini.

Mgonjwa mwenye maradhi haya kama ugonjwa utatokea mapafu yake yatashindwa kufanya kazi ipasavyo hivyo kusikia maumivu makali kifuani ambayo kitaalam huitwa acute chest syndrome.

Tatizo lingine ambalo mgonjwa atapata ni figo zake kushindwa kufanya kazi kutokana na kuathirika ama maji kupungua mwilini, hivyo mgonjwa kupata tatizo la kutopata mkojo sawa sawa.

Mgonjwa pia atakuwa na tatizo la hatari la damu yake kushindwa kwenda kwenye ini, tendo ambalo kitaalam huitwa sequestration.

Aidha, wanaume wanaokuwa wameathiriwa na ugonjwa huu watakuwa wakihisi maumivu kila wanaposimamisha uume na kitendo hicho kitaalam huitwa priapism.

Wagonjwa wengi wenye sickle cell macho yao huathirika na kuwa na kiwango kidogo cha chembechembe za damu (red cell) mwilini.

Mtu mwenye ukosefu wa chembechembe nyekundu za damu huwa rahisi kukumbwa na ugonjwa wa anemia.

Aidha, mtu mwenye ugonjwa huu akipata mtoto mchanga ukuaji wake unakuwa wa taratibu ukilinganisha na watoto wengine ambao hawana maradhi haya.

Ugonjwa huu mara nyingi hauna tiba wala chanjo. Wataalamu wanasema mgonjwa mwenye matatizo haya akifikisha miaka 15 anaweza kujikuta akiwa hana tatizo hilo.

Au hata kama analo basi anaweza kujisikia nafuu mno kwa sababu tatizo litakuwa halijitokezi mara kwa mara au linaweza lisijitokeze tena.

USHAURI

Kwa kuwa ugonjwa huu huathiri figo ambazo zinaweza kushindwa kufanya kazi, au damu kushindwa kwenda kwenye ini na mgonjwa kushindwa kupata mkojo vizuri, inashauriwa ikiwa una mgonjwa mwenye tatizo hilo awe anakwenda kupimwa mara kwa mara.

Leave A Reply