The House of Favourite Newspapers

Airtel, Axieva Washirikiana na Kampuni ya Bima ya Alliance Kuzindua Bima Kidigitali

0
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini (TIRA) Khadja Said (wa pili kulia), Mkurugenzi Mwenza wa Axieva Africa Gaurav Dhingra (wa pili kushoto) wakiwa na Mkurugenzi wa Huduma za Airtel Money Isack Nchunda (kulia) na Anantha Krishnan, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Alliance (kushoto) wakionyesha alama ya Airtel Bima mara baada ya kuzindua ushirikiano baina ya kampuni hizo tatu ambao utawawezesha wateja wa Airtel kwa sasa wanaweza kununua bima ya gari binafsi pamoja na biashara kupitia simu ya mkononi.

 

 

Dar es Salaam, Tanzania – Jumatano 23 Marchi, 2022: Wateja wa Airtel kwa sasa wanaweza kununua bima ya gari binafsi pamoja na biashara kutoka na ushirikiano baina ya Airtel Money Limited, kampuni ya bima ya Alliance na mtoa huduma wa teknolojia wa BIMA Axieva Africa Lab Limited. Huduma hiyo itajulikana kama Airtel BIMA na itakuwa kwenye orodha ya huduma za Airtel money kwa kupiga *150*60# , ni moja kati ya huduma bora na ya haraka ambayo unaweza kununua bima ya gari yako kwa kutumia simu ya mkononi ndani ya sekunde 60 na ukapata papo hapo vithibitisho vyako vyote vya malipo  kama vile a sera, kibandiko cha stika pamoja na risiti ya TRA ya EFD.

Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Airtel Tanzania Isack Nchunda akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla hiyo.

 

Kupitia huduma ya Airtel BIMA  itasaidia wateja kuepuka usumbufu wa kutembea safari ndefu, usumbufu wa kutembea na pesa taslimu na changamoto ya kubeba makaratasi kutafuta huduma ya bima kwa ajili ya magari yao badala yake wanaweza kupiga *150*60# kwenye simu zao za Airtel muda wowote na kupata menu ya BIMA inayotolewa na kampuni ya bima ya Alliance papo hapo. Ikiwa chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini – TIRA, kampuni ya Alliance ni mtoa huduma za bima kwa upande wa magari namba 1.

Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Airtel Tanzania Isack Nchunda.

 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza ushirikiano huu, Kaimu Kamishna wa TIRA Khadja Said ameipongeza kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuzindua huduma hii.

“Naomba kuchukua fursa hii kuwapongeza kampuni ya Airtel Tanzania, kampuni ya Bima ya Alliance na wenzao Axieva kwa juhudi zao za pamoja na kuweza kuzindua huduma hii ambayo ni ya kimapinduzi kwa utoaji wa bima kidigitali. Kwa kupitia mpango huu, Watanzania wengi wataweza kupata huduma za bima wakati wowote, mahali popote kwa kutumia simu zao”.

Anantha Krishnan, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Alliance akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

Said aliongeza, “Lengo letu ni kuendelea kupenyeza huduma za bima kwa kuongeza uhamasishaji na matumizi ya bima kutoka asilimia 15 ya sasa mpaka asilimia 50 mpaka kufika mwaka 2030. Tunafurahia ushiriki wa wadau kama huwa wa kutumia teknolojia katika kufikia dhamira na malengo yetu”’.

Vile vile, kampuni ya bima ya Alliance na Axieva kwa pamoja wamefanya kazi kubwa kufanikisha mageuzi haya makubwa kwenye sekta hii, alisema Said.

Mkurugenzi wa huduma za Airtel Money Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema, “Tunayo furaha kuleta mageuzi haya kabambe ya Airtel Money BIMA kidigitali kwa kupitia ubunifu tulionao kuptia Airtel Money, niwahakikishie wateja wetu kuwa ushirikiano huu na Axieva pamoja na kampuni ya bima ya Alliance wakuleta huduma za bima kidigitali ni mwanzo wa hatua kubwa wa kuja na huduma nzuri zaidi ya hapa .

Huduma za bima, hadi sasa imesalia kuwa mojawapo ya huduma  ambazo hazipewi kipaumbele kutoka na hali ya mlolongo mrefu ya upatikanaji wake, na malipo ya huduma hii mara nyingi hutumia makaratasi. Hivyo kwa kutumia huduma ya Airtel Money pamoja na ushirikiano huu wa miundo mbinu, tunaondoa vikwazo vyote hivi kwa wateja wetu na kuweza huduma ya bima kwa kugusa kifute tu.

Nia yetu ni kuhahakisha Watanzania wote milioni 60 wanapata huduma ya Airtel BIMA ili waishi maisha ya Uhuru zaidi, aliongeza Nchunda.

Anantha Krishnan, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya bima ya Alliance alisema, “Uzinduzi huu wa ushirkiano baina ya Airtel Tanzania na Axieva ni matokeo ya dira ya pamoja ya mabadiliko ya sekta hii na upatikanaji wa huduma za bima kidigitali kwa kila mtumiaji.

Imekuwa ni dhamira yetu kuwaweka wateja wetu kwanza, na kuwaletea ubunifu ambao ni wa kwanza sokoni na huduma ambazo zinapatikana kwa urahisi. Ni Imani yetu kwamba kwa kuzindua huduma hii ya USSD kama msambazaji utaongeza thamani kubwa kwa wateja wote, kwa kampuni ya Alliance, sekta ya bima na nchi kwa jumla.

Kwa hakika leo ni siku ya kihistoria! Na tunajivunia sana, kwamba leo kwa ruhusa kutoka TIRA, ambaye ni mdhibiti tunapeleka huduma za bima kwenye ngazi nyingine ambapo nchi zingine zitatamani kujifunza kutoka Tanzania.


Kwa upande wake, Gaurav Dhingra, Mkurugenzi mweza Axieva Afrika, kampuni ambayo inaendesha teknolojia ya Axieva BIMA alisema,
 “Dhamira yetu sisi Axieva ni kutengeneza mifumo yenye teknolojia endelevu, na ambayo inaweza kuleta matokeo chanya na kuwezesha  jamii kupata huduma bora kupitia teknolojia.

 

Kwenye menu ya Airtel BIMA, hakuna haja ya kujisajili. Mtumiaji anaweza tu kupiga menu ya Airtel Money *150*60# na kufuata orodha iliyo chini ya huduma za kifedha za Airtel Money ili kupata huduma za bima zilizoidhinishwa na TIRA kwa bima za magari, pikipiki na bajaji, alisema Dhingrwa wakati akionyesha jinsi ya kutumia huduma hii kwa simu za mkononi.

Leave A Reply