The House of Favourite Newspapers

Saido, Moloko Wavuruga Mipango Yanga

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amepanga kuliboresha eneo la winga ndani ya kikosi chake ambalo limeonekana kuwa na upungufu mkubwa.

Kauli hiyo aliitoa Jumamosi iliyopita mara baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kumalizika kwa Yanga kushinda 2-0 dhidi ya KMC, uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Yanga hivi sasa inakosa huduma ya viungo washambuliaji, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ na Jesus Moloko ambao wapo nje ya uwanja wakiuguza majeraha, wakitarajiwa kurejea kabla ya mchezo dhidi ya Azam FC, Aprili 6, mwaka huu.

Akizungumza na Spoti Xtra, Nabi alisema katika kikosi chake, eneo la winga ambalo hivi sasa linachezwa na Chico Ushindi na Denis Nkane, limeonekana kutotimiza majukumu yake vizuri ya kutengeneza mabao.

Nabi alisema mawinga hao waliocheza dhidi ya KMC, walishindwa kutimiza majukumu yao ya kupiga krosi kwa mshambuliaji, Fiston Mayele.

Aliongeza kuwa, anaamini katika mchezo ujao dhidi ya Azam eneo hilo litacheza vizuri ambalo amepanga kuliboresha mara baada ya timu hiyo kuingia kambini.

“Tulichelewa kuingia mchezoni na wenzetu walitumia udhaifu huo dakika 20 za mwanzo. Bahati haikuwa upande wao la sivyo wangepata si chini ya mabao mawili.

“Lakini umakini mkubwa wa golikipa wetu Diarra (Djigui) na mabeki uliweza kutuokoa kufungwa kipindi cha kwanza ambapo hatukuwa na utulivu mzuri hususani eneo la kiungo na winga.

“Nimeliona tatizo hilo, hivyo nitalifanyia kazi mazoezini mara baada ya timu kuingia kambini kujiandaa na mcheo ujao dhidi ya Azam ambao huenda nikawatumia baadhi ya mawinga niliokuwa ninawatumia akiwemo Saido ambaye amepona majeraha ya goti,” alisema Nabi.

STORI NA WILBERT MOLANDI | CHAMPIONI JUMATANO

UTATA! MREMA KUOA BINTI MDOGO MWEUPE, PADRI ANASEMAJE KUHUSU NDOA? HAYA HAPA MAJIBU…

Leave A Reply