The House of Favourite Newspapers

Airtel Kugawa Faida ya 2.1/- Bilioni kwa Wateja Wake wa Airtel Money

0
Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda akitoa habari hiyo njema kwenye mkutano na wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya Kampuni Airtel, Dar.

 

 

Dar es Salaam Alhamisi 13 Januari 2022:  Airtel Tanzania  imetangaza kuanza kutoa faida ya TZs. 2,011,886,007 bilioni kwa wateja wa Airtel Money Zaidi ya 10 milioni, ikiwa ni sehemu ya faida iliyopatikana kwenye akaunti za Airtel Money kwa kipindi cha Julai mpaka Septemba 2021.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutangaza kuanza kutoa faida kwa wateja wa Airtel Money, Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda, alisema, “tuna furaha kubwa sana kuona kuwa huduma ya Airtel Money inaendelea kuwa msingi wa shughuli za kibiashara hapa nchini. Tuko katika mchakato wa kugawa Shilingi bilioni 2,011,886,007 kwa wateja wetu ambao wamekuwa wakitumia mfumo wetu kwa kipindi hiki, na malipo yanaingia moja kwa moja katika akaunti zao za Airtel Money.”

Faida italipwa kwa wateja, mawakala, wakala mkuu na wadau wengine wa kibiashara wa Airtel Money kulingana na matumizi yao ya huduma za Airtel Money. Faida linategemea kiasi cha matumizi ya huduma katika kipindi hicho cha Julai mpaka Septemba 2021. Shughuli hizo ni pamoja na kuhamisha pesa, kulipa bili, manunuzi ya muda wa maongezi na mengine.

Mara baada ya kupokea faida yake, wateja wa Airtel Money wanaweza kutumia faida hilo kwa njia ya kutoa pesa taslimu, kununua vifurushi vya maongezi na data au kutumia kulipia bili au manunuzi ya bidhaa.

Mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda (kushoto) na Meneja Chapa wa Airtel wakiendelea kuwajuza wanahabari taarifa za kugawa faida hiyo kwa wateja wake. 

 

 

Nchunda aliongeza, “Mfumo huu wa kipekee umekuwa na nafasi kubwa katika kujenga hali ya ushirikishwaji na upatikanaji wa huduma za kifedha nchini. Wanawake na vijana wameona unafuu na urahisi wa kutumia Airtel Money na wanatumia huduma nyingi ili kuboresha maisha yao. Pia mfumo umekuwa rasilmali muhimu katika kuwezesha biashara ndogo ndogo. Kwetu Airtel Tanzania, dhamira yetu ni kuhakikisha kuwa mfumo huu unaendelea kuwa mfumo unaoendana zaidi na mahitaji ya wateja.”

Leave A Reply