The House of Favourite Newspapers

Airtel Kukabidhi Msaada kwa Waathirika wa Mafuriko Iringa‏

0

01Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Simu za Mkononi nchini Airtel Kanda ya Nyanda za Juu, Bw. Straton Mushi (kushoto) akimkabidhi jana Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bw. Richard Kasesela msaada wa saruji mifuko 100 na mabati 200 vyenye thamani ya Tsh. milioni 5 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko Pawaga na Idodi wilaya ya Iringa. (Picha na mpiga picha wa Airtel).

2Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bw Richard Kasesela (kulia ) akipokea msaada wa bati 200 pamoja na saruji 100 vyote vikiwa na thamani ya Tsh. milioni 5 kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Bw. Straton Mushi jana msaaada uliotolewa kwa ajili ya waathirika wa mafuriko Pawaga na Idodi wilaya ya Iringa (picha na Francis Godwin).3Bw. Richard Kasesela (kushoto mwenye suti) akimpomngeza Bw. Straton Mushi kwa niaba ya kampuni hiyo simu za mikononi kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Pawaga na Idodi Iringa. (Picha na mpiga picha wa Airtel).

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel jana imetembelea wahanga wa mfuriko ya mvua katika jimbo la Isimani, Wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa na kuwapatia msaada wa mahitaji muhimu kwaajili ya ujenzi wa makazi baada ya makazi yao ya awali kuzoewa na mafuriko. Zaidi ya familia 220 zimepoteza makazi kufatia mvua kubwa iliyonyesha mwishoni mwa Februari mwaka huu.

Akiongea wakati wa makabithiano ya msaada huu, Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bwana Straton Mushi alisema” Tunaungana kwa pamoja katika maafa haya na kutoa pole kwa familia zilizoathirika na mafuriko haya.

Tunatambua pia mafuriko haya yamewaacha wakazi wengi bila makazi, huku mazao yao ya chakula na biashra kuharibiwa na mifugo yao kufa hivyo tunaungana kwa pamoja na wakazi wa Iringa vijijini ili kuwawezesha kujenga makazi yao upya. Leo kwa niaba ya Airtel kupitia ofisi yetu ya kanda ya juu kusini tunatoa msaada wa mabati 200 na saruji mifuko 100 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5 na kuwaomba watanzania kuungana nasi kuwasaidia ndugu zetu wa Isimani ili kuepuka milipuko ya magonjwa isitokee. Pia huu ni wakati muhimu wa kushirikiana kuwawezesha wenzetu kurudi na kukaa na familia zao ili kufanya shughuli zao za kawaida mapema iwezekanavyo.

Akiongea kwa niaba ya wakazi wa Isimani, Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela Alisema “Tunawashukuru sana Airtel kwa msaada huu umekuja wakati tunauhitaji zaidi, napenda kuwaomba watanzania kushiriki kwa kuchangia na kwa makampuni mengine kujitolea na kutusaidia katika hali ngumu ambayo imetuweka kwenye hatari kupata milipuko ya magojwa na zaidi tumekosa makazi na shughuli zetu za kiuchumi zimeteketea. Tunawashukuru waliojitolea mpaka sasa na tunaomba muendelea na moyo huo wa kujitolea.

Leave A Reply