The House of Favourite Newspapers

Airtel na Benki ya Letshego Wakabidhi Zawadi Washindi wa Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba

0
Mshindi wa kwanza wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba Emmanuel Lugakingira (kushoto) akifurahi na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Majanga wa Benki ya Letshego, Mbajo Mchomvu.   

 

 

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo kwa kushirikiana na benki ya Letshego wamekabidhi zawadi kwa washindi  wa droo ya mwisho ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba.

Promosheni hiyo ambayo ilikuwa ni ya wiki sita, ilikuwa na lengo la kuhamashisha Watanzania kujiwekea utaratibu wa kujiwekea Akiba.

 

Washindi hao ni Emmanuel Lugakingira mkazi wa Mikocheni Dar es Salaam ambaye amekabidhiwa milioni tano na Nigwike Kibona ambaye amekabidhiwa milioni moja.

 

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo, Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza washindi hao kwa kushinda na pia kwa kujiwekea Akiba.

 

Kampeni hii ya Weka Akiba Ushinde na Airtel Timiza ilikuwa na lengo la kuhamashisha utamanduni wa kuweka akiba kwa wateja wa Timiza Akiba na vile vile kuwavutia wateja wengine wapya. Tunaendelea kutoa wito kwa Watanzania kuendeleakujenga utamanduni wa kuweka akiba alisema Nchunda huku akiongeza kuwa Airtel Tanzania imeshirikiana na benki ya Letshego kuendesha kampeni hii”.

 

 

 

Meneja Uhusiao wa Airtel Tanzania Plc Jackson Mmbando (kushoto), akimkabidhi mshindi wa kwanza wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba Emmanuel Lugakingira ambaye ailijishindia Tzs 5 milioni. Promosheni hiyo ambayo ilikuwa ya wiki sita ilikuwa na lengo la kuhamashisha Watanzania kuwa na utamanduni wa kujiwekea Akiba huku ikiendesha kwa ushirikiano wa Airtel Tanzania na benki Letshego. Katikati Mkuu wa Kitego cha Majanga (Risk) Letshego Mbajo Pius Mchomvu.                                                                                             

 

 

 

Mkuu wa Kitego cha Majanga (Risk) Letshego Mbajo Pius Mchomvu akimkabidhi mshindi wa pili wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba Nigwike Kibona ambaye alijishindia Tzs 1 milioni. Promosheni hiyo ambayo ilikuwa ya wiki sita ilikuwa na lengo la kuhamashisha Watanzania kuwa na utamanduni wa kujiwekea Akiba huku ikiendesha kwa ushirikiano wa Airtel Tanzania na benki Letshego. Kati kati ni Meneja Uhusiano Airtel Jackson Mmbando.

 

 

Meneja Uhusiao wa Airtel Tanzania Plc Jackson Mmbando (katikati), akimtambulisha mshindi wa kwanza wa droo kubwa ya promosheni ya Weka Akiba Ushinde na Timiza Akiba, Emmanuel Lugakingira (kushoto) ambaye aliyejishindia Tzs 5 milioni kulia ni Mkuu wa Kitego cha Majanga (Risk) Benki ya Letshego, Mbajo Pius Mchomvu.                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                              
Leave A Reply