The House of Favourite Newspapers

Airtel na TFF Yapanga Mikakati ya Maendeleo ya Soka la Vijana

0

IMG_6140  Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmando akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa maendeleo ya mpira wa miguu nchini uliokutanisha Kampuni ya Airtel pamoja na Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF). Kulia ni Katibu Mkuu TFF Celestine Mwesigwa na kushoto Afisa Habari TFF Alfred Lucas.

IMG_6145Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Celestine Mwesigwa akiongea wakati wa kikao cha maendeleo ya mpira wa miguu nchini kati ya Airtel Tanzania na TFF. Kulia ni Mhasibu Mkuu wa TFF Daniel Msangu na Kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.

Dar es Salaam, Jumatano Mei 18 2016 Kampuni ya Airtel Tanzania leo imekutana na Shirikisho la Mpira Tanzania (TFF) kuzungumzia mipango ya maendeleo wa mpira wa miguu nchini ikiwa ni pamoja na michuano ya vijana chini ya umri 17 ya Airtel Rising Stars inayotarajiwa kuanza Juni mwaka huu.

Katibu Mkuu wa TFF Celestine Mwesigwa ambaye ndio aliongoza kikao hicho, alitoa shukrani ka kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la vijana ambalo ndio msingi wa kukuza mpira wa miguu nchini. Naamini ya kwamba kwa kuendelea kuwekeza kwenye soka la vijana, tutaweza kufika mbali kwa kupata matokeo mazuri.

Tangu kuanzisha kwa michuano ya Airtel Rising Stars miaka mitano iliyopita, soka la vijana nchini imekuwa na mafanikio makubwa. Leo, Timu ya Taifa chini ya miaka 20 – Serengeti Boys, imeundwa na vijana ambao wamekuwa ni chimbuko la Airtel Rising Stars, alisema Mwesigwa na kuongeza kuwa hata timu ya Taifa ya Wanawake – Twiga Stars, Klabu za Liguu na zile zinazoshiriki ligi daraja ya kwanza, zinatumia wachezaji ambao wamekuzwa kwa michuano ya Airtel Rising Stars.

Airtel imeweza kuiwezesha TFF kufika maeneo ambayo yamekuwa ni vigumu kufika kutafuta vipaji. Kwa kufanya hivyo, tuweza kupata vijana wenye vipaji vingi na hata kwa sasa hivi, baadhi yao wako na Timu ya Taifa ya Vijana Serengeti kushiriki michuano ya Kimataifa inayoendelea India, alisema Mwesigwa.

Katibu Mkuu huyo wa TFF aliomba Airtel kuendelea kudhamini miradi ya soka ya vijana kwa vile ndio njia pekee Tanzania inaweza kuwa na timu bora na imara ya Taifa. Nchi nyingi zinazofanya vizuri kwenye michuano mbali mbali ya soka ni kwa vile waliweza kuwekeza kwenye program mbali mbali za vijana kama vile Airtel Rising Stars. Kwa kushirikiana na nyinyi, tutaweza kupata na kukuza vipaja vya soka ambazo watakuwa na msaada mkubwa kwenye timu ya Taifa.

Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “kampuni yake itaendelea kudhamini program za soka la vijana ambazo zimeweza kuwa na mafanikio makubwa kwa miaka mitano iliyopita. Lengo letu ni kuwa na timu ya taifa bora kama vile Misri, Cameron, Nigeria, Ivory Coast na Ghana, alisema Mmbando huku akisisitiza njia pekee ya kufikia mafanikio hayo ni kuwekeza na kukuza soka la vijana.

Airtel pia imetoa shukrani kwa Serikali kupitia Wizara ya Habari, Michezo na Sanaa pamoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushirikiano wao ambao umeifanya Airtel Rising Stars kuwa moja ya mashindano yenye mafanikio makubwa hapa Tanzania. Bila ushirikiano na serikali pamoja na wadau wa soka hapa nchini, Airtel Rising Stars hangeweza kufika hapa ilipo kwa leo, alisema Mmbando.

Mmbando alisema kwa mwaka huu, Tanzania haitashiriki kwenye michuano ya kimataifa ambayo huleta pamoja wachezaji waliong’ara kwenye nchi zao Barani Afrika kwa ajili ya kubadilisha uzoefu, bali itashirikiana na TFF kuweka mikakati  mingi zaidi ya kuwawezesha vijana hawa kufanya vyema hata baada ya mashindano ya Airtel Rising Stars kwisha.

Leave A Reply