The House of Favourite Newspapers

Airtel Yagawa Bilioni 1.7 kwa Watumiaji wa Airtel Money

Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari. Hawapo pichani.
kutoka kushoto ni Meneja wa Huduma za Airtel Money, Ibrahim Malando, Isack Nchunda na Jackson Mmbando.

 

 

KAMPUNI simu ya Airtel Tanzania leo Januari 18, mwaka huu imetangaza kugawa neema ya pesa za Kitanzania Shilingi Bilioni 1.7 kama gawio la faida kwa wateja wake hapa nchini wanaotumia huduma ya Airtel Money pamoja na mawakala wa Airtel Money.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, leo Januari 18, 2017, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isack Nchunda amesema pesa hizo zitagawiwa kwa wateja wake wanaotumia huduma ya Airtel Money pamoja na mawakala wa Airtel Money nchi nzima. Amesema hii ni mara ya tano kwa Airtel Money kugawa gawio la faida kwa wateja wake tokea mwaka 2015 ambapo Mr. Money hurudisha kwa wateja wake gawio hilo kulingana na salio linalosalia katika akaunti ya mteja kila siku.

 

Aidha, amefafanua kuwa hadi kufikia leo, jumla ya shilingi Bilioni 13 zimeshagawiwa kwa wateja mbalimbali wa Airtel Money kama gawio.

 

Kwa upande wake Meneja wa Huduma za Airtel, Ibrahim Malando amesema kila mteja wa Airtel Money atapata gawio lake kuanzia leo hii na kisha kuamua matumizi ya pesa yake mwenyewe, ikiwa ni pamoja na kununua bando, muda wamaongezi, au kufanya malipo ya huduma mbalimbali kama vile LUKU, na kadhalika.

 

Malando amesema Mawakala wa Airtel Money nao watapokea sehemu ya gawio hili kama kawaida kwa awamu nakusisitiza waendelee kuwahudumia wateja wa Airtel ili kujiongezea faida zaidi kwa gawio lijalo. Katika hatua nyingine Malando amesema Airtel imejipanga kutoa huduma ya Airtel Money kwa gharama nafuu na salama zaidi huku akidai kukua kwa huduma hiyo kwa siku za hivi karibuni kama inavyoonekana kwenye ripoti ya Huduma za Fedha kwa Mtandao iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano TCRA.

 

Airtel wanaendelea kutoa huduma nafuu na rahisi kwa wateja wake ambapo kwasasa kutuma pesa kuanzia shilingi 200, 000 na kuendelea ikiwa ni Bure kabisa. Sanjari na hayo Airtel pia hutoa huduma ya mkopo iitwayo TIMIZA, mkopo ambao hauna masharti yoyote ili kuwawezesha wateja wake kutimiza malengo mbalimbali waliyojiwekea.

 

Airtel money pia imeungana na taasisi za biashara zaidi ya 400 na benki zaidi ya 30 pamoja na kuongezeka kwa idadi ya mawakala zaidi elfu 50 ili kurahisisha huduma za kifedha mjini na vijijini.

 

NA DENIS MTIMA | GPL

Comments are closed.