The House of Favourite Newspapers

Aishtaki Serikali kwa Kumfunga Kizazi kwa Lazima

Mwanamke mmoja nchini Japan, ambaye alilazimishwa kufungwa kizazi miaka ya 1970 akiwa na umri wa miaka 15, ameishitaki serikali katika kesi ya kwanza ya aina yake.

Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina lake ni mmoja wa wanawake 25,000 waliopitia upasuaji wa kuwafungwa kizazi chini ya sheria ambayo kwa sasa haitekelezwi.

Waathiriwa walifungwa kizazi kwa sababu walibainika kuwa na magonjwa ya kiakili ama wenye matatizo kama vile ukoma.

Mwanamke huyo ambae kwa sasa ana umri wa zaidi ya miaka 60, alichukua hatua ya kisheria baada ya kubaini kuwa alifungwa kizazi chake mwaka 1972 baada ya kupatikana na maradhi ”ya urithi ya kasoro ya ubongo”.

 

Taarifa zinasema mwanamke huyo anataka alipwe fidia ya $101,000 (ZAIDI YA TSH. 224.7) kwa uharibifu huo aliotendewa kwenye mwili wake, akielezea kwamba haki zake kama binadamu zilikiukwa.

Comments are closed.