The House of Favourite Newspapers

JPM Awalipua Majaji ‘Wala Bata’, Atoa Maagizo Mazito

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamisi Juma kupitia Tume ya Utumishi wa Mahakama iliyo chini yake kuwachunguza baadhi ya Majaji ambao wamekuwa wakiomba likizo na kusafiri Ulaya kwa zaidi ya siku 28 wakila na kunywa kuhko na familia zao.

 

Raid Magufuli ameyasema hayo leo Februari 1, 2018 wakati akihutubia kwenye kilele cha sherehe ya wiki ya sheria nchini iliyofanyika jijini Dar es salaam.

 

“Kuna baadhi ya watumishi katika sekta ya sheria maadili yao yamepungua, hii ni kweli na ni lazima niseme, wapo wachache.

 

“Katika vibali vya likizo vinavyoombwa na majaji, wapo baadhi yao wanakwenda Ulaya na Afrika Kusini lakini wanaandika watajigharimia wenyewe, lakini wanakaa huko siku 28 au 30 na familia zao wakila kwenye hoteli kubwa kubwa, hizo pesa wanazitoa wapi, nani anawadhamini? Mimi sina majibu, naomba tume yako Jaji Mkuu ichunguze.

 

“Wapo baadhi watumishi wa mahakama wanaomba rushwa, wanabambikiza kesi wananchi, wanachelewesha kesi, wanaharibu upelelezi, wanachelewesha kuandika kesi na kupendelea. Lakini unaweza kushangaa miongoni mwao walikuwemo mahakimu 26 na walipopelekwa mahakamani wote wakashinda, hakuna hata mmoja aliyepatikana na hatia.

 

“Naipongeza tume ya maadili kuwastaafisha au kuwachukulia hatua watumishi hawa, shughulikia kwa kuwastaafisha na kuwachukulia hatua kwa manufaa ya umma wakiwemo mahakimu 14 waliofukuzwa kazi na wengine 64,” alisema Magufuli.

 

 

 

Comments are closed.