The House of Favourite Newspapers

Ajali ya Colombia: Ndege Ilichelewa Kupata  Mafuta Kituo Kilichofuata

 

1

Mabaki ya ndege iliyoanguka nchini Colombia ikiwa na wachezaji wa klabu ya Chapocoense ya Brazil.

2

Eneo la milima ilipoanguka ndege hiyo na kuua watu 71.

3

Miili ya waliopoteza maisha katika ajali hiyo ikitolewa eneo la tukio.

4

Wachezaji wa Chapecoense wakipozi na rubani wa ndege iliyoanguka, Miguel Quiroga.

5

Shabiki wa Chapecoense akisoma ujumbe wa maombolezo kwa wachezaji waliopoteza maisha.

6

Wachezaji ambao hawakusafiri na timu wakiwalilia wenzao.

7

Bodi ya wakurugenzi wa Klabu ya Chapecoense wakiwa Medellin ambapo miili ya wachezaji ilipelekwa.

9

Majeneza yenye miili ya marehemu waliopoteza maisha katika ajali hiyo.

NDEGE iliyoanguka nchini Colombia ikiwa na wachezaji wa klabu ya Chapocoense ya Brazil ikielekea nchini humo kwa ajili ya mchezo wa soka mwanzoni mwa wiki hii, inasemekana ilichelewa kuondoka na hivyo kuchelewa kupata mafuta katika kituo kilichofuata kwa vile wafanyakazi wake walikuwa wakitafuta kidude cha michezo ya video cha mchezaji mmoja ambacho kilikuwa hakionekani.

Kuchelewa huko kulisababisha ndege hiyo ambayo ilikuwa ipate mafuta kwenye mpaka kati ya Brazil na Bolivia, ishindwe kufanya hivyo kwa vile kituo hicho cha ndege huwa hakifanyi kazi usiku.

Ndege hiyo iliyokuwa imebeba wachezaji wa klabu ya Chapecoense kwenda kwenye fainali ya kombe la nchi za Amerika ya Kusini (Sudamericana Copa) ilibidi isubiri kwenye uwanja wa ndege wa Medellin lakini iliishiwa mafuta kabla ya kutua hapo.

Ndege hiyo ilianguka mlimani na kuua watu 71 ambapo ilikuwa imesafiri kwa dakika 20 zaidi kuliko muda wake wa kawaida wa saa nne kabla ya kujaza tena mafuta.

Inasemekana rubani wa ndege hiyo, Miguel Quiroga ndiye aliyefanya kosa kwa kuamua kwenda moja kwa moja Medellin bila ya kujali kuweka mafuta huko Bogota, nchini Bolivia.

Ndege hiyo yenye kusajiliwa kama BAE 146 Avro RJ85, ikiwa na injini za jeti, uwezo wake wa kusafiri ikiwa na mafuta ni maili 1,600, umbali ambao ni kati ya mji wa Medellin na Santa Cruz nchini Bolivia.

Katika tukio hilo, rubani alifanya kosa kwa kufikiri kwamba mafuta aliyokuwa nayo yangemfikisha Medellin.

halotel-strip-1-1

Comments are closed.