The House of Favourite Newspapers

Ajali ya Moro: Waanua Matanga Baada ya Kumwona ‘Marehemu’

FAMILIA ya mzee Humphrey Mongi, mkazi wa Kihonda jini Morogoro hivi karibuni ililazimika kuanua matanga waliyoyaweka baada ya kugundua kwamba kijana wao, James Mongi (30), waliyeamini amefariki kwenye ajali ya moto uliotokea mjini humo kutokana na gari lililokua na mafuta, alikuwa hai.

 

Akizungumza na mtandao huu baba mzazi wa James, Mzee Mongi alisema kijana wake anaishi kata ya Mwembesongo, jirani kabisa na eneo ilipotokea ajali hiyo ambapo baada ya janga hilo hakuonekana na kutokana na miili iliyokuwa imeungua vibaya, ambapo  walishindwa kutambua mwili waliohisi ni wake, hivyo wakajua alikuwa miongoni mwa waliofariki bila kujulikana.

“Mimi namfahamu mwanangu kwa namna alivyo,  nilihisi lazima angekuwepo kwenye tukio hilo,” alisema mzee Mongi na kuongeza kwamba baadaye  katika kumtafuta, kutokana na ushauri wa watu, walimkuta akiwa mikononi mwa vyombo vya usalama (Magereza) kutokana na kushikwa akiwa anavuta bangi sehemu ya Msamvu.

 

Baada ya hapo msiba uligeuka na kuwa sherehe.

Mzee Mongi anamiliki gereji jirani na kanisa la KKKT Usharika wa Mji Mpya.

STORI: DUNSTAN SHEKIDELE

Comments are closed.