The House of Favourite Newspapers

Breaking: Tundu Lissu Ashinda Pingamizi

ALIYEKUWA Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, ameshinda pingamizi la Serikali ya Tanzania dhidi ya maombi yake ya kibali cha kufungua kesi kupinga kukoma kwa ubunge wake baada ya Spika Job Ndugai kumvua ubunge.

 

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Agosti 26,2019 na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Jaji Sirillius Matupa. wakati akitoa  uamuzi wa pingamizi la awali dhidi ya maombi ya Lissu lililowekwa na Serikali katika maombi yake ya kibali cha kufungua shauri ili kupigania ubunge wake.

 

Lissu alifungua maombi Mahakama Kuu, Masjala Kuu, Dar es Salaam chini ya hati ya dharura, kupitia kwa kaka yake Alute Mughwai ambaye amempa mamlaka ya kisheria kufanya hivyo, ikiwa ni hatua ya awali kabisa ya kupigania kurudishiwa ubunge wake alioukosa tangu Juni 28, 2019.

 

Kesi hiyo inatokana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai kufuta ubunge wa Lissu siku zaidi ya 60 zilizopita kwa maelezo kuwa hajulikani alipo na hakusaini fomu za maadili. Katika kesi hiyo  Serikali ya Tanzania ina mawakili  15 dhidi ya wanne wa Lissu.

Comments are closed.