The House of Favourite Newspapers

Ajali Yaua 25 Singida

1

ajali singida (9) ajali singida (10) ajali singida (11)

Watu 25 wamefariki dunia, huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya mabasi mawili kugongana huko wilayani Manyoni mkoani Singida.

Mabasi hayo yanayomilikiwa na Kampuni ya City Boy, moja lilikuwa linasafiri kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Kahama na lingine lilikuwa linatoka Kahama kwenda Dar es Salaam.

Akizungumzia ajali hiyo, Kamanda wa Polisi  mkoani Singida, Thobias Sedoyeka amesema idadi ya majeruhi bado haijajulikana japo kuwa amesema ni wengi.

“Ni kweli ajali imetokea Manyoni na tupo eneo la tukio tunaendelea na utaratibu wa kuondoa majeruhi na miili pamoja na mabasi haya barabarani,”  amesema Kamanda Sedoyeka.

1 Comment
  1. Jaffari yogo says

    Poleni Sana wafiwa wote na majeruhi wote wa ajali hii. Madereva wawe makini sana barabarani ili kuepuka ajali.

Leave A Reply