The House of Favourite Newspapers

Ajali yaua 50 Ghana

0

ajali ghana

Takriban watu 50 wamefariki dunia katika ajali mbaya ya barabarani kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka mingi.

Basi moja lililokuwa limejaa abiria liligongana uso kwa uso na lori lililokuwa limebeba nyanya huko kaskazini mwa nchi hiyo jana jioni.

Rais wa Ghana, John Mahama ameielezea ajali hiyo kama ”habari mbaya” katika mtandao wake wa twitter na kuongeza kuwa huduma ya kukabiliana na masuala ya dharura inakabiliana na hali hiyo.

Baadhi ya walionusurika wamewaambia polisi kwamba breki za lori hilo zilifeli, lakini kiini cha ajali hiyo bado kinachunguzwa.

Leave A Reply