The House of Favourite Newspapers

AJIBU AJICHELEWESHA KUSUDI YANGA

Staa wa Yanga, Ibrahim Ajibu

STAA wa Yanga, Ibrahim Ajibu amepewa bonge la mchongo kwamba ana uwezo halisi wa kwenda kusakata soka barani Ulaya kama ilivyo kwa staa wa KRC Genk, Mbwana Samatta lakini safari hiyo anaitia ugumu mwenyewe kwa sababu bado hajaamua kufanya hivyo.

 

Kauli hiyo ya Ajibu kupelekwa kwenda kucheza soka Ulaya imetolewa na kocha wa mchezaji huyo, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo ambaye anaamini kabisa nyota huyo anajichelewesha tu kuendelea kucheza soka hapa Bongo.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Zahera amesema kwamba; “Yeye ni mchezaji ambaye anastahili kabisa kwenda nje kucheza soka na siyo hapa Tanzania kwa sababu ni aina ya wachezaji ambao wanahitajika sana kwani ana kipaji halisi cha soka tofauti na wachezaji wengi.

 

“Lakini atashindwa kucheza huko kwa sababu moja tu ya kushindwa kujitoa na kutumia nguvu wakati akiwa uwanjani. Ni yeye mwenyewe ambaye anajichelewesha kwenda kucheza nje kwani hastahili kucheza hapa kwa sababu ya jambo hilo la kushindwa kujitoa zaidi nje ya uwezo wake,” alisema Zahera.

 

Ajibu amefanya mambo makubwa msimu huu baada ya kuhusika kwenye mabao 11 ya timu hiyo na sasa ndiye mchezaji anayetajwa zaidi kuwa ni bora kwenye ligi.

Habari na Said Ally | Championi

Comments are closed.