The House of Favourite Newspapers

Ajibu Habari Nyingine, Aweka Simba, Yanga

0

IBRAHIM Ajibu, kiungo mshambuliajiwa Simba ni habari nyingine Bongo, kwani anashikilia rekodi kwa washambuliaji wa Simba na Yanga kwa kuwa mzawa pekee kutoka katika timu hizo kongwe aliyefunga bao kwenye michuano ya Azam Sports Federation’s Cup (ASFC), maarufu kama Kombe la FA.

Simba na Yanga ni timu ambazo zimefunga jumla ya mabao 10, mabao 9 yamefungwa na wachezaji wa kigeni huku bao moja tu likifungwa na mzawa Ajibu.

 

Desemba 21, nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi raia wa Congo aliiongoza timu yake kwenye ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Iringa United Uwanja waUhuru. Tshishimbi alifunga bao moja huku mengine yakifungwa na Lamine Moro raia wa Ghana, Mnyarwanda, Patrick Sibomana aliyetoa asisti mbili kwenye mchezo huo na David Molinga raia wa Congo.

Simba ilishinda mabao 6-0 mbele ya Arusha United  Desemba 22, wafungaji wakiwa ni Gerson Fraga raia wa Brazili, Deo Kanda raia wa Congo, FrancisKahata raia wa Kenya, Clatous Chama raia wa Zambia, Meddie Kagere raia wa Rwanda na Ibrahimu Ajibu akiwa mzawa pekee aliyefunga bao kwenye mabao 10 yaliyofungwa na timu hizo ambazo zinatarajiwa kumenyana Januari 4, mwakani Uwanja wa Taifa, Dar.

 

Ajibu alitoa asisti mbili katika mchezo huo, hivyo akawa amehusika kwenye mabao matatu. Mohamed Hussein, ‘Mmachinga’ mshambuliaji wa zamani wa Yanga na Simba ameliambia

Championi Jumatano kuwa kuna tatizo kubwala ushambuliaji kwa wazawa, jambo linaloiliza hata timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Stori: Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Leave A Reply