The House of Favourite Newspapers

Bosi Championi Amtunuku Njumu Staa wa Yanga Princess – Video

0
Fatuma Bushiri, (Cynthia) baada ya kukabidhiwa viatu na Saleh Jembe.

    

MHARIRI Mtendaji wa Global Publishers inayomiliki magazeti namba moja kwa michezo nchini, Championi na Spoti Xtra, Saleh Ally ‘Jembe’ ametoa zawadi ya njumu pea mbili kwa kiungo fundi wa timu ya Wanawake Yanga Princess, Fatuma Bushiri, (Cynthia).

 

Jembe alitoa zawadi hiyo leo Jumanne katika Ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori Jijini Dar, ikiwa kama sehemu ya kumtia moyo mchezaji huyo mkongwe kweye soka la Wanawake, Tanzania kufuatia kuzihakiwa mitandaoni na wadau mbalimbali wa soka nchini juu ya muonekano wake na viatu vya mpira alivyovaa.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Cynthia alisema: “Namshukuru bosi Saleh kwa kuguswa na kile kilichotokea juu yangu na kuamua kufanya kitu kama hiki kama sehemu ya kunitia Moyo, kiukweli nimekuwa na furaha ambayo siwezi kuilezea, kupewa pea mbili za viatu ni deni kubwa kwangu ambalo natakiwa kulilipa kwa kufanya kazi bora uwanjani.”

 

Kwa upande wa Saleh alisema: “Niliguswa sana baada ya kuona watu wakimzungumzia vibaya Cynthia heti kwa sababu ya muonekano, bila kujali kuwa amekuwa sehemu ya mafanikio ya soka la Wanawake nchini kwa zaidi ya miaka 10.

 

Mhariri Mtendaji wa Global Publishers, Saleh Ally (kulia) akimkabidhi Cynthia viatu.

 

“Hawa watoto ambao wanaonekana sasa wanacheza huyu ni mtu ambaye ametengeneza njia lakini mbali na hilo bado anacheza kwa kiwango cha juu na amekuwa msaada kwa timu ya Taifa Twiga Stars kwa kipindi chote hicho.

 

“Hivyo nilimtafuta na kuzungumza naye na kuamua kumpa hiki kitu japo siyo kikubwa sana, lakini kitamtia Moyo yeye mwenyewe na kujua kumbe kuna watu wanafahamu mchango wangu kwenye soka la Wanawake, lakini kubwa zaidi itumike kama somo kwa watu wengine kwa kutomjaji mtu kwa sababu ya muonekanao wake,” alisema Saleh.

 

Issa Liponda

 

Mchezaji YANGA QUEENS Aliyelizwa na MANARA Apewa VIATU Vipya!

Leave A Reply