The House of Favourite Newspapers

AJIBU: ZAHERA ANANIPA HASIRA ANAPONISEMA

MKALI wa asisti ndani ya Ligi Kuu Bara, Ibrahim Ajibu ambaye mpaka sasa amefikisha tisa akiwa na mabao matatu amesema kuwa kwake moto hauzimi kutokana na maneno ambayo anaambiwa na kocha Mkuu Mwinyi Zahera kumpa hasira zaidi.

 

Zahera amekuwa akimwambia Ajibu kuwa bado haonyeshi juhudi akiwa uwanjani licha ya kuwa msaada akiwa ndani ya uwanja jambo ambalo limekuwa likipokelewa kwa utofauti na Ajibu.

“Maneno yake huwa yananiumiza moyo lakini yananipa hasira na nguvu ya kupambana hasa nikiwa uwanjani hata nje ya uwanja bado najifunza muda wote ili kuwa bora zaidi ya jana nikiwa ndani ya uwanja.

 

“Ushindani ni mkubwa kwa sasa nasi tunajitahidi kufanya vizuri na yote yanawezekana kwa kuwa tumeshatengeneza muunganiko mzuri ambao unatusaidia tupate matokeo mazuri na hilo ni jambo la faraja kwetu, mashabiki watupe sapoti,” alisema Ajibu ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba.

Viungo washambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu na Mrisho Ngassa jana asubuhi wameripoti kwenye mazoezi ya timu hiyo huku wakikanusha taarifa za kugomea mazoezi.

 

Katika mazoezi ya juzi wachezaji wanne wa timu hiyo Ajibu, Andrew Vicent ‘Dante’, Matheo Antony na Mrisho Ngassa hawakuonekana katika mazoezi huku taarifa zikienea wameweka mgomo kwa kile kilichodaiwa ni madai ya mishahara yao ya miezi minne wanayodai. Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh alisema wachezaji hao walikuwa na matatizo tofauti.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Comments are closed.