The House of Favourite Newspapers

Ajira Zaidi ya 5,000 Kutengenezwa Kutoka Kiwanda cha Sukari Mkulazi, Morogoro

0

Kukamilika kwa kiwanda cha kuzalisha Sukari Mkulazi kilichopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kumetajwa kuwa kutawezesha kutoa ajira za moja kwa moja na za muda mfupi kwa vijana zaidi ya 5000.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mwamini Juma Malemi alipokuwa katika ziara ya kutembelea na kukagua kiwanda hicho ambacho hadi sasa kimekamilika kwa asilimia 100 na tayari kimeanza kazi.

Aidha alisema kuwa sukari inayozalishwa katika kiwanda hicho itaanza kupatikana madukani hivi karibuni na pia kutakuwa na duka maalumu litakalouza sukari kwa bei elekezi ya kiwanda.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mkulazi, Dk. Heridelita Msita alisema kuwa kiwanda hicho kimeanza kazi na kuwahakikishia Watanzania upatikanaji wa sukari ya kutosha kutoka kwenye kiwanda hicho.

Hata hivyo, alisema kuwa hadi sasa kuna baadhi ya makampuni yamekuwa yakiweka oda  kwa ajili ya kupata sukari inayozalishwa katika kiwanda hicho ambacho kimekuwa na manufaa makubwa kwa wananchi na vijana kwa kupata ajira na kujiongezea kipato chao.

Leave A Reply