The House of Favourite Newspapers

AJIUA KIKATILI KISA PENZI LA BINAMU YAKE – VIDEO

MTU mmoja mkazi wa Makumbusho Kijitonyama jijini Dar es Salaam amejinyonga kwa kamba hadi kufa chumbani kwake  kwa kilichoelezwa kua ni kisa cha mapenzi na nduguye aliyekataa kuolewa naye.

Katika barua aliyoiacha, marehemu amelalamika kwamba aliacha familia yake mke pamoja na watoto watatu akiamini kwamba atamuoa huyu binti alyempenda. Baada ya muda wakiwa kwenye mahusiano, mwanamke kageuka na kusema hawawezi kuoana sababu ni ndugu.

Jambo hilo lilisababisha kuchukua maamuzi ya kujiua ambapo mwili wake umechukuliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi. Judith Karumba, ambaye afisa mtendaji wa Makumbusho kathibitisha tukio hilo. 

SHUHUDIA TUKIO HILO

Comments are closed.