The House of Favourite Newspapers

LEMA Ataka Gavana wa B.o.T Ajiuzulu, Sababu Ziko Hapa – Video

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amepinga hoja za Gavana wa Benki Kuu,Profesa Florens Luoga kuwa walitumia askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) katika operesheni ya maduka ya kubadili fedha, kwa kuwa kulikuwa na uhaba wa polisi.

 

BoT iliendesha operesheni ya kukagua maduka ya kubadilisha fedha mjini Arusha ikitumia maofisa wake na askari wa JWTZ mapema wiki hii, jambo ambalo limepingwa na wadau ambao wanasema jeshi liachwe lifanye kazi zake.

 

Lema, ambaye alikuwa mmoja wa watu walioandika mtandaoni kuonya dhidi ya matumizi hayo ya wanajeshi, amewaambia waandishi wa habari leo (Novemba 21) kuwa ni kosa kubwa kutumia jeshi katika mambo ya kiraia.

LEMA Amvaa JPM Ataka Gavana Ajiuzulu

Comments are closed.