The House of Favourite Newspapers

Akiba Commercial Bank Washerehekea Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja

0
Mkurugenzi Mtendaji akikabidhi cheti cha mfanyakazi bora katika nyanja ya utoaji huduma kwa Immaculata Hamulungi wa tawi la Ubungo Plaza.

 

 

5.Oktoba.2022: Dar es Salaam; Benki ya Akiba Commercial Bank washerekea wiki ya  huduma kwa wateja katika matawi yao mbalimbali toka kuanzishwa kwa benki hiyo miaka 25 iliyopita.

 

Akizungumza katika kusherekea wiki hiyo ya huduma kwa wateja Mkurungezi Mtendaji bwana Silvest Arumasi amesema ni muhimu kusherekea wiki hiyo ya huduma kwa wateja kwani ni namna ya kuwasherekea na kuwathamini wateja wake ambao wamekua nao katika safari yao kama benki ya biashara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc ndugu Silvest Arumasi akikata keki na wateja na wafanyakazi wa Benki ) ya akiba mapela leo alipoungana kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja pamoja na wateja katika tawi letu la Ubungo Plaza.

 

Kauli mbiu ya maadimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka huu ni ‘Furahia huduma’  au ‘Celebrate service’ ambayo ni namna ya kuwaenzi wateja wetu kuwa tutaendelea kuwahudumia kwa viwango vya juu na kiweledi ili kukidhi kiu ya kupata huduma bora .Swala la kuhakikisha wateja wetu wanafurahia huduma ni kipaumbele kwetu.

Mmoja wa wafanyakazi wa Akiba Commercial akimkabidhi zawadi mteja wa benki hiyo.

 

Benki ya Akiba Commercial Bank wamekuwa na utamaduni wa kusherekea wiki ya huduma kwa wateja kama namna ya kutoa shukrani kwa wateja vilevile kukusanya maoni na mirejesho kutoka kwa wateja hao.

Picha ya pamoja ys wafanyakazi wa Benki ya Akiba tawi la Ubungo.

 

Akiendelea kuzungumza Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank bwana Silvest Arumasi alisema wateja wengi waliomba kuongezewa idadi ya mawakala na mawakala hao wameongezwa na kufikia idadi ya jumla ya mawakala 2000 na zaidi.Vilevile kulikua na maombi ya uboresha huduma ya kutuma na kutoa fedha ndani na nje ya nchi, huduma ya mikopo ikijumuisha muda wa kupewa mkopo, muda wa kurejesha, aina ya dhamana na aina mbalimbali ya mikopo yote yamefanyiwa kazi ikiwemo kuongezwa kwa mikopo ya waajiriwa wa serikali na sekta binafsi. Mbali na hapo pia wajiriwa wote wana uwezo wa kupata ‘salary advance’ nayotolewa kwa ajili ya dharura na fursa zinazo jitokeza papo kwa papo.

 

‘’Huduma nyingine iliyoingia sokoni ni bima ya maisha, rasilimali,vikundi n.k ambazo zitapatikana katika matawi yetu yote na fidia hutolewa kwa muda mfupi. Benki pia imepanua wigo wake na kuwafikia wateja wakubwa na taasisi za umma ambapo huduma zitatolewa kwa kuzingatia mahitaji ya wateja husika hivyo natoa rai kututembelea ili kupata fursa hizo.’’

 

Kwa kuzingatia umuhimu wa kutoa huduma bora kwa ajili ya kuwaridhisha wateja wetu Benki imeboresha tarabu za uendeshaji kwa kuanzisha kitengo mahsusi cha huduma kwa wateja ambacho kinafuatilia kwa karibu kero nachangamoto za wateja na kufanya utatuzi wake ndani ya muda mfupi iwezekanavyo. Pia katika matawi yetu yote kuna afisa mahusiano ambao huakikisha kuna mahusiano kati ya Benki na wateja.

 

Mmoja wa wateja wa Akiba Commercial Bank, Bwana  Issa Nkya ambaye ni Mkurungezi wa Mabasi ya Happy Nation benki hiyo kwa. kuwathamini wateja wake na kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja na pia kufanya uboreshaji katika huduma zake mbalimbali ikiwemo uboreshwaji katika huduma za miamala ya fedha na kuongeza idadi ya mawakala ambazo huwasaidia katika majukumu yao ya kila siku.

 

Mwisho, kabisa alimaliza kwa kusema kuwa Benki inaendelea kuimarisha na kuboresha mifumo yake ya utoaji huduma pamoja na kuboresha na kuanzisha huduma mpya. Lakini kwa kuzingatia umuhimu wa wateja.

 

‘’Napenda kusema kuwa pamoja na kupokea maoni na mirejesho kupia kitengo cha huduma kwawateja, Benki yetu huwa ina utamaduni wa kupima viwango vya uridhikaji yaani “customer satisfaction” kutokana na huduma zetu kwa kufanya kwa kutumia kampuni binafsi isiyokuwa na maslahi yoyote na Benki kwa lengo la kupata picha na mrejesho halisi kuhusiana na huduma zetu. Hii inaitwa Independent Customer Satisfaction survey ambayo inafanyika kila mwaka kama nilivyosema lengo nikujua hali halisi ya huduma zetu pamoja na viwango vya uridhikaji kwa lengo la kufanya maboresho zaidi’’.

 

Hivyo anawakaribisha wote katika maadhimisho haya ya wiki ya huduma kwa wateja kwa kusema ‘Celebrate Service’ au ‘Furahia Huduma’.

Leave A Reply