The House of Favourite Newspapers

Akil The Brain Alamba Dili Specious Afrika

0
Msanii aliyewahi kutamba na vibao vingi kwa staili ya Bhangra, Akil The Brain akizungumza na waandishi wa habari.
Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.

 

MSANII aliyewahi kutamba na vibao vingi kwa staili ya Bhangra, Akil The Brain leo hii amelamba dili katika lebo ya muziki ya Specious Afrika.

 

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Akil aliyewahi tamba na vibao kama Regina na Bongo Bhangra alisema huu ni mwanzao wa kuleta mapinduzi na kwamba alikuwa kimya tangu 2013 na sasa amerudi upya.

 

“Najiona kama nimezaliwa upya. Wote mnanifahamu kwa jinsi nilivyo kwenye kuimba. Nimerudi na mapinduzi mapya katika muziki. Nawapongeza Specious Afrika kwa kuniweka kundini tena,” alisema Akil.

 

Naye mkurugenzi wa Specios Afrika ambaye pia ni msanii, prodyuza na mtangazaji, Hennesseyy alisema kuwa, baada ya kufanikisha Specious sehemu mbalimbali ikiwemo Amerika sasa ni zamu ya Afrika.

 

“Tumejipanga, tumesoma muziki wa Tanzania na kuona unafaa kufanya kitu cha kitofauti kwa hiyo niwaambie tu waandishi wa habari Specious Afrika inarudi kivingine na mtarajie kuona mambo mengi.

 

“Tayari tuna msanii Elly Da Bway na Akil The Brain na tunategemea kutanuka zaidi ya hapa. Elly Da Bway ameshaachia nyimbo mbili mpaka sasa, wa kwanza ni Boss na sasa ameachia Sura ambao umeshaanza kutikisa. Akil naye yupo mbioni kuachia,” alisema Hennessey.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply