The House of Favourite Newspapers

Zitto Akamtwa Tena, Ahamishiwa Kituo Cha Polisi Kamata – Video

0
Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe.

KIONGOZI  wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe baada ya kukamatwa leo asubuhi nyumbani kwake kwenda  kuhojiwa katika kituo cha polisi Chang’ombe jijini Dar es Salaam  kutokana na hotuba yake katika Kata ya Kijichi, ambapo  aliachiwa,  amekamatwa tena kwa amri ya ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Zitto aliyeachiwa kwa dhamana na kukamatwa tena, amepelekwa kituo cha polisi cha Kamata kwa mahojiano zaidi kuhusu tuhuma za kutoa lugha za kichochezi.

Maneno hayo yaliyopelekea Zitto kushikiliwa na kuhojiwa ni pamoja na kusema: “Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kufanya uchunguzi na kuwakamata watu waliompiga risasi Mbunge Tundu Lissu…

Wananchi wasiichague CCM kwa sababu Serikali yake imeshindwa kueleza chanzo cha miili ya watu wanaookotwa kwenye fukwe za bahari kama Coco Beach. Hivyo kuichagua CCM ni sawa na kuwaunga mkono waliofanya vitendo vya kumshambulia Tundu Lissu na wanaoua watu wanaookotwa kwenye fukwe.

Msimamo wa ACT-Wazalendo Baada ya Zitto Kabwe Kukamatwa!!!

Leave A Reply