The House of Favourite Newspapers

Alichokisema Tundu Lissu Leo Hoteli ya Protea

0
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) Tundu Lissu akiongea na wanahabari.

MWANASHERIA Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) Tundu Lissu, leo ameongea na waandishi wa habari katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam akisindikizwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na Mjumbe wa Kamati Kuu, Frederick Sumaye ambapo miongoni mwa mambo mengi aliitaka serikali kufafanua juu ya mambo kadhaa.

 

Aliitaka serikali kuelezea kuhusu ndege ambayo ilitakiwa kuwasili nchini Julai mwaka huu ambapo hadi sasa haijafika.  Kwa mujibu wa Lissu, alitaja sababu za kutofika kwa ndege hiyo ambayo ni kukamatwa ndege hiyo aina ya Bombadier Q400 kwa sababu Tanzania inadaiwa fedha na kampuni ya Stirling Civil Engineering Ltd ambayo iliomba kibali na kupewa kutoka Mahakama Kuu ya Montreal kukamata mali zozote za Tanzania zitakazokuwa nchini Canada.

 

Lissu aliyasema hayo na kusisitiza kwamba serikali na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa hajasema lolote kuhusu suala hilo.

 

Miongoni mwa mambo mengine aliyoyasema ni kuvitaka vyombo vya dola kufanya kazi zake inazotakiwa kwa maslahi ya taifa na si kwa kuwafuatilia watu wasiokuwa na hatia, hususani wanasiasa.


Leave A Reply