The House of Favourite Newspapers

Aliko Dangote alivyomaliza ugomvi wa Don Jazzy na Olamide

0

imageOlamide  akipeana mkono na Don Jazzy.

DURU za muziki hivi sasa zinafahamu kwamba bifu lililokuwepo kati ya wasanii, Olamide na Don Jazzy, wote wa Nigeria, ambalo lilianzia katika tamasha la utoaji tuzo la Headies Award, ambapo mshindi wa jumla hujinyakulia gari, hivi sasa limemalizika.

Ugomvi huo uliokuwa wa maneno, ulikolezwa na kituo cha televisheni cha Live International na kusambaa hadi kwenye mtandao wa Twitter.
Hata hivyo, swali kubwa ambalo mashabiki walikuwa wakijiuliza ni kwamba: Nani aliumaliza ugomvi huo baina ya nyota hao?

10881Jibu lake ni kwamba: Mwafrika tajiri kuliko wote, ambaye ni raia wa Nigeria pia, Aliko Dangote, ndiye aliyemaliza bifu hiho. Inaelezwa zaidi kwamba picha ya Olamide na Don Jazzy wakishikana mikono, ilichukuliwa katika makazi ya Dangote, na hili lilitokea baada ya Olamide kumwomba msamaha Jazzy – yote hayo yakiwa ni juhudi za Dangote.

Katika majibizano yaliyokuwa katika Twitter, Don Jazzy na kundi lake hawakusema neno lolote; ni kwa sababu Don alikuwa amekasirishwa sana na tukio lililozua bifu hilo, hususani kwa vile Olamide alikuwa

Leave A Reply