The House of Favourite Newspapers

Aliyejibadilisha Kuwa Mzee Anaswa Marekani

0

mzee

Shaun “Shizz” Miller.

Polisi nchini Marekani wamemkamata mtoro mmoja baada ya kugundua kuwa alikuwa akidanganya kuwa yeye ni mtu mzee.

Polisi walizingira nyumba moja huko Massachusetts na kumuamrisha Shaun “Shizz” Miller atoke nje.

Kisha akatoka nje akiwa amejibadilisha na kuwa kama mtu mzee, lakini wakati akitoka polisi waligundua kuwa alikuwa ni yule yule waliyekuwa wakimtafuta mwenye umri wa miaka 31 na kumkamata.

Amekuwa mafichoni tangu ashtakiwe kwa kuhusika kwenye ulanguzi wa madawa ya kulevya mwezi Aprili.

Wakati polisi walisaka nyumba hiyo walipata bunduki mbili na karibu dola 30,000 pesa taslimu.

Leave A Reply