The House of Favourite Newspapers

ALIYEJIFYATUA MDOMO KWA RISASI APANDIKIZWA USO MPYA

JAMAA mmoja wa Yuba City, California nchini Marekani, Cameron Underwood amerejeshewa furaha yake na sasa anaweza kutabasamu baada ya kufanyiwa upasuaji na kumpandikiza uso mwingine.

Underwood (26) ambaye Juni 2016 alifanya jaribio la kujiua kwa kujipiga risasi mdomoni na kuharibu uso wake mzima huku akipoteza pua yake, amesema watu waliokuwa wakimtazama usoni walikuwa wakipigwa na butwaa.

 

“Sasa nina pua na mdomo, kwa hivyo ninaweza kutabasamu, kuongea na kula chakula kigumu tena, ninashukuru sana kwa upasuaji huu wa kupandikizwa uso kwa sababu imenipa fursa ya pili ya maisha,” alisema Underwood.

 

Jamaa huyo ambaye sehemu kubwa ya chini ya mdomo na meno yake yote viliondoka isipokuwa moja tu katika kisa hicho anasema; “Nimefanikiwa kurejea shughuli nyingi ninazozipenda kama kukaa nje, kushiriki michezo na kutumia muda na marafiki na familia yangu. Nina matumaini ya kurudi kazini karibuni na wakati mmoja kuwa na familia.

Januari mwaka huu, zaidi ya madaktari na wahudumu wengine wa afya 100 walichukua muda wa saa 25 kumfanyia upasuaji Cameron kwenye kituo cha afya cha NYU Langone huko Manhattan, New York na taarifa za kupona kwake zilifichuliwa wiki hii.

 

Jeraha hilo limepona ikiwa ni miezi 18 bada ya jaribio la Cameron kutaka kujiua ambao kituo hicho kinasema ndio muda mfupi zaidi kati ya jeraha na upasuaji katika hostoria ya Marekani. Tangu upasuaji wa kwanza wa kupandikizwa uso mwaka 2005, zaidi ya upasuaji mwingine 40 umefanyika kote duniani.

Upasuaji huo uliongozwa na Dr Eduardo D. Rodriguez ambaye anasema kando na hatua kubwa za matibabu, ni moyo wa kutaka kuishi aliokuwa nao Cameron ulifanikisha upasuaji huo. Upasuaji wa Cameron ndio wa tatu kufanywa na Dr Rodrigues na anasema kuwa muda mfupi ambao Cameron alikuwa ameishi na majeraha pia ilikuwa sababu kuu ya kupona kwake.

“Cameron hajaishi na majeraha yake kwa muongo mmoja au zaidi kama vile watu wengine,” alisema.

Kutokana na hilo hukuweza kukumbwa na matatizo mengine ya kisaikolojia jambo ambalo husababisha madhara kama msongo wa mawazo, matumizi ya madawa ya kelevya na tabia zingine zenye madhara. Wakati wa upasuaji, daktari alijenga upya sehemu za chini za mdomo na pua na kurejesha meno yote 32.

BAVICHA Wazungumza Muda HUU

Comments are closed.