The House of Favourite Newspapers

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Dkt. John Pima na Wenzake Washinda Rufaa ya Kupinga Kifungo cha Miaka 20

0

Watumishi watatu waliokuwa Waajiriwa wa Serikali katika Jiji la Arusha ambao ni Mkurugenzi wa Jiji, Dkt. John Pima, Innocent Maduhu aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji, na aliyekuwa Mweka Hazina wa Jiji, Mariam Mshana wameachiwa huru baada ya kushinda rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela

Akitoa uamuzi huo, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Fredrick Lukuna, amesema Mahakama ya chini haikuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi inayomhusu mteule wa Rais bila kibali maalumu cha Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP), hivyo kufuta hukumu iliyowatia hatiani.

MCHUNGAJI MASHIMO AFUNGUKA MAYELE KUTUPIWA MAJINI na YANGA – AONESHA USHAHIDI wa VIDEO | MPAKA HOME

Leave A Reply