The House of Favourite Newspapers

Kiongozi wa upinzani Russia Navalny aaga dunia akiwa jela

0
Aliyekuwa kiongozi wa upinzani mwenye umri wa miaka 47 Alexey Navalny.

Maafisa wa magereza nchini Russia wanasema kiongozi wa upinzani mwenye umri wa miaka 47 Alexey Navalny, ameaga dunia.

Taarifa rasmi haijaweza kuthibitishwa na vyanzo huru.

Vyombo vya habari vya Russia vimewanukuu maafisa kadhaa wa Huduma za Magereza za Serikali Kuu wakisema Navalny, kiongozi machachari wa upinzani hasimu wa Rais Vladimir Putin, alifariki Ijumaa huko katikatik mwa Russia baada ya kuwa mgonjwa alipokuwa akitembea.

Wanasema kuwa madaktari waliitwa lakini hawakuweza kumuokoa baada ya kupoteza fahamu.

Maafisa wanasema uchunguzi umeanzishwa kufahamu chanzo kilchopelekea kifo cha kongozi huyo wa upinzani.

Navalny alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 19 jela kwa mashtaka ya msimamo mkali sana.

Alihamishwa kutoka jela ya zamani alikokuwepo katika mkoa wa Vladimir katikati ya Russia na kwenda katika jela yenye ulinzi mkali huko mjini Kharp, katika mkoa wa Yamalo-Nenets, kiasi cha kilomita 1,900 kaskazini mashariki mwa Moscow.

MCHUNGAJI MASHIMO AFUNGUKA MAYELE KUTUPIWA MAJINI na YANGA – AONESHA USHAHIDI wa VIDEO | MPAKA HOME

Leave A Reply