The House of Favourite Newspapers

Aliyemuua Mkewe na Kumfukia Alikusudia, Afunguka A-Z – Video

Simanzi bado imetawala katika Kijiji cha Mkwalia, Tarafa ya Mkuranga mkoani Pwani kufuatia tukio la kikatili la mwanadada Rosemary Magombora (43) kuuawa na mumewe kisha kufukiwa katika shimo lililopo jirani na nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe.

 

Rosemary, muuguzi mfawidhi msaidizi wa Hospitali ya Mkuranga, inadaiwa kuwa alipigwa na mumewe Robert Mgombela hadi kufariki kisha mwili wake kufukiwa katika shimo hilo, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda, wawili hao walikuwa wakihitilafiana mara kwa mara, hadi kufikia hatua ya kupigana kwa kile mwanaume alichokuwa akidai kwamba mwanamke huyo hakuwa mwaminifu kwenye ndoa yao.

 

Inadaiwa kwamba Rosemary ambaye alikuwa ni muuguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, alitendewa ukatili huo na mumewe, Machi 21, mwaka huu lakini mwili wake ulikuja kupatikana Mei 25, mwaka huu ukiwa tayari umeshaharibika.

 

SHUHUDIA TUKIO HILO

Comments are closed.