The House of Favourite Newspapers

Aliyetemwa Simba Agombewa Sauzi, Zambia

0
Moses Phiri

KLABU ya Amazulu FC ya nchini Afrika Kusini sambamba na Zesco  United, Red Arrows na Power Dynamos zote za Zambia zimeingia katika vita ya kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Moses Phiri ambaye ameachiwa kwa mkopo.

Phiri ni kati ya wachezaji walioachwa katika usajili wa dirisha dogo la Januari, mwaka huu ambalo limefungwa hivi karibuni ili kutoa nafasi ya kulinda kipaji chake.

Nyota huyo ameondolewa kikosini baada ya kukosa nafasi ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo kinachonolewa na Abdelhak Benchikha.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka Simba mshambuliaji huyo upo uwezekano wa kusaini Power Dynamos kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita ambao ukimalizika atasini mkataba wa kudumu hapo.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mshambuliaji huyo amezigomea Amazulu, Zesco na Red Arrows kutokana na ofa kiduchu aliyopewa kabla ya kuchukua maamuzi ya kusaini Power Dynamos.

 

“Muda wowote, Power Dynamos wanatazamia kukamilisha na kutangaza usajili wa mshambuliaji Phiri.

“Na atajiunga na Power kwa mkopo kutoka Simba hadi mwisho wa msimu huu akiwa na kipengele cha kuufanya mkataba wake huo kuwa wa kudumu.

“Phiri mwenyewe amekubali kusaini Dynamos, ambayo yeye ndiyo anaona inafaa kwenda kupambania namba na kuingia katika kikosi cha kwanza,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Phiri tumemuachia aondoke kwa mkopo wa miezi sita, bado hajatupa taarifa wapi anakwenda, lakini uongozi tumetoa baraka za yeye kujiunga na timu yoyote.”

STORI NA WILBERT MOLANDI

ONA ANAPOISHI ‘BABY ZUU’ – ”NINA USICHANA WANGU – NAOGA MARA 7 – WANAUME ACHENI USHAMBA”…

Leave A Reply