The House of Favourite Newspapers

Aliyetobolewa Macho Na Scorpion Atishiwa Kuuawa -Video

0


Siku chache zilizopita, Global TV ilifanya mahojiano na Said Mrisho, mhanga wa tukio la kuchomwa visu kisha kutobolewa macho na Salum Njwete almaarufu Scorpion akieleza jinsi maisha yake yalivyobadilika baada ya tukio hilo lililotokea miaka mitano iliyopita katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani jijini Dar es Salaam.

 

Kwa kipindi chote hicho, Scorpion anaendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka saba aliyohukumiwa gerezani huku tetesi zikieleza kwamba yupo kwenye hatua za mwisho kuachiwa kwa msamaha wa parole.

 

Hata hivyo, muda mfupi baada ya mahojiano hayo aliyoyafanya Said na waandishi wetu, Richard Bukos na Issa Mnally, yameibuka malalamiko mapya kutoka kwa Said, akidai kwamba kuna watu wamekuwa wakimpigia simu na kumtishia maisha yake. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply