The House of Favourite Newspapers

Aliyewezeshwa na Airtel Fursa atoa ajira kwa vijana wengine 15

0

PICT 1 Kijana Innocent Kipondya aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akimuonyesha Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya ziwa Emmanuel Raphael mazao aliyepota baada ya kuwezeshwa, alipotembelewa shambani kwake hapo jana.

PICT 2Kijana Innocent Kipondya aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akibeba mazao aliyofuna baada ya kuwezeshwa miezi 11 iliyopita.

PICT 3Kijana Innocent Kipondya (juu ya Toyo) aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa kuwawezesha vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel FURSA Tunakuwezesha akiwa anaelekea sokoni baada ya kufuna mazao yako na kupata faida na kuweza kuajiri vijana wengine 15.

 

Mwanza, 21 Juni 2016, Mafanikio ya Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kuhakikisha Kijana mkulima mdogo aliyewezeshwa na Airtel  kupitia mpango wake wa Airtel FURSA Tunakuwezesha  ameweza kuongeza ukubwa wa shamba, mazao na kuajiri wengine yameanza kuonekana baada ya mkulima mdogo Innocent Kipondya wa kijiji cha Mwalogwabagole wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza  kuajiri vijana wenzake 15 shambani kwake.

Kupata mafanikio kwa Innocent kunafuatia miezi 11 iliyopita Airtel FURSA kumwezesha pampu ya kuvuta maji na mpira wake, ikiwa ni pamoja na bajaji kwa ajili ya kusafirisha mazao sokoni.

Innocent amesema ilikuwa inampa wakati mgumu kulima wakati wa kiangazi lakini sasa anaweza kulima wakati wote kwa kumwagilia kutokana na pampu ya kuvuja maji aliyowezeshwa na Airtel FURSA.

“ Kabla sijashikwa mkono na Airtel Fursa nilikuwa napata changamoto ya mazao kukauka kutokana na maji kuwa mbali, lakini sasa licha ya kupanua kilimo, nina uhakika wa kulima mwaka mzima” amesema Innocent

Innocent amemwambia mwandishi wa habari hii kuwa, soko la nyanya ni la uhakika na sasa ameamua kulima mbogamboga na kupanua kilimo cha mpunga, japo kuwa wadudu waharibifu ni kikwazo kwake kupata mazao mengi zaidi.

Ameipongeza Airtel kwa kuwajali vijana hapa nchini, na sasa amefanikiwa kusimamisha jengo na baadaye ana mpango wa kununua wanyama kazi  kwa ajili ya kulima.

Meneja Masoko wa Airtel Kanda ya ziwa Emmanuel Raphael ,mbali na kumpogeza Innocent kwa bidii aliyoionyesha alipomtembelea, amesema dhana ya kampuni yake ni kuendelea kuinua vijana na  wajasiliamali wadogo hapa nchini ili kuweza kubadilisha maisha yao.

“Miezi 11 nilikuja hapa, shamba la nyanya lilikuwa moja tu,lakini sasa naona mashamba manne,bustani ya mbogamboga,kilimo cha mpunga hata vitungu,nampongeza sana Innocent” aliongeza Emmanuel

Airtel Fursa ni mradi wa kijamii wenye lengo la kuhamasisha vijana, kuwapa fursa ya kujiendeleza kibiashara na kuwapa ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao katika mikoa yote nchini

Leave A Reply