The House of Favourite Newspapers

Alliance wanunua mabao ya Yanga

KATIKA kuhakikisha wanapata ushindi, Uongozi wa Alliance FC umeweka wazi kwamba hawataki utani kwenye mechi yao dhidi ya Yanga ndiyo maana wametenga milioni kadhaa kwa kila mchezaji atakayefunga bao leo Jumamosi.

 

Alliance ambao waliweka kambi nchini Rwanda wakijiandaa na mechi hiyo, wataikaribisha Yanga leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Alliance, Jackson Mwafulango alisema kuwa wamejipanga kuifunga Yanga inayonolewa na Kocha Mwinyi Zahera kuhakikisha hilo linafanikiwa tayari wametenga mamilioni kwa mchezaji yeyote atakayefunga bao.

 

“Tumejipanga kiasi cha kutosha, kambi ilikuwa nzuri, uwekezaji wetu pia ni mkubwa, sasa wachezaji wote wameambiwa kwa kila atakayefunga milioni yake imetengwa pembeni, sasa hapo kazi ni kwao hata wafunge mabao 11, milioni zao zinawasubiri lengo ni kuhakikisha tunafika mbali,” alisema Mwafulango.

Lunyamadzo Myuka, Dar es Salaam

Comments are closed.