The House of Favourite Newspapers

Magufuli Atunuku Kamisheni Maofisa 146 JWTZ – Video

Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akikagua gwaride la heshima la maofisa-wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kabla ya kuwatunuku kamisheni maofisa wapya 146 wa kundi la 65 la mwaka 2018 katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

AMIRI Jeshi Mkuu Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, akikagua gwaride la heshima la maofisa-wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kabla ya kuwatunuku kamisheni maofisa wapya 146 wa kundi la 65 la mwaka 2018 katika viwanja wa Ikulu jijini Dar es Salaam.

…Akiwa katika nafasi yake wakati wa hafla hiyo.

Maafisa hao wametunukiwa ukamishna baada ya kupata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi mkoani Arusha yaliyoanza Machi 12 mwaka 2018.

Waliotunukiwa kamisheni na Rais Magufuli ni maafisa wapya wa JWTZ kundi la 65 kwa mwaka 2019 ambapo jumla yao ni 146, kati yao 140 ni wanaume na sita ni wanawake.

Ma0fisa-wanafunzi wa JWTZ wakivalishana vyeo mara baada ya kutunukiwa kamisheni.

…Wakila kiapo cha utii.

Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi mkoani Arusha, Bregadia Jenerali Steven Mkande amesema kati ya idadi hiyo ya maafisa waliotunukiwa kamisheni watatu wana shahada ya uzamili, 116 wana shahada ya kwanza na mmoja ana stashahada ya uzamili.

Rais  Magufuli akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF) Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi cha Monduli, Brigedia Jenerali Steven Mnkande (kulia)  wakati wakienda kupiga picha za kumbukumbu.

Stashahada ya juu ina maafisa watatu huku madaktari wakiwa 23 kati yao 21 ni madaktari wa kawaida wa binadamu na wawili ni madaktari wa wa kinywa na meno.

…Akiwa na wakuu wa JWTZ na maofisa wapya aliowatunuku kamisheni.

PICHA NA IKULU

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ikiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan; Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Comments are closed.