Athumani Hemed (kushoto) mkazi wa Tandale sokoni akijaza kuponi kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba. Anayemshuhudia ni Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.
Selemani Amir (kulia) akipewa maelekezo na Mkanda namna ya kujaza kuponi yake.
Juma Kambi (wa pili kulia) akijaza kuponi yake.
Omary Hatibu akijaza kuponi kushiriki droo kubwa ya bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
Mhina Salum (kulia) akijaziwa kuponi na Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda.
Mkanda akizidi kuwasaidia kujaza kuponi zao wasomaji wa gazeti la Amani ili kushiriki bahati nasibu hiyo.
Yahya Ramadhan akisaidiwa kujaza kuponi na Mkanda.
…Akimtajia namba yake ya simu Mkanda ili iandikwe katika kuponi hiyo.
Fred Peter (kulia) akishiriki kujaza kuponi ya bahati nasibu.
Hussein Kadudu (kushoto) akijaza kuponi, anayemshuhudia ni Yohana Mkanda.
Mkanda akimjazia kuponi mdau wa gazeti la Amani aliyejitambulisha kwa jina la Abbas Fundi.
…Akimwelekeza msomaji wa gazeti la Amani, Ally Mohammed, namna ya kujaza kuponi ili kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
BAHATI nasibu ya ‘Shinda Nyumba’ ikiwa imebakiza siku chache tu kuchezeshwa leo Alhamisi promosheni ya shindano hilo iliwafikia wakazi wa Tandale na maeneo mengine jijini Dar waliojitokeza kwenye gari la matangazo walipochangamkia kununua Gazeti la Amani na kushiriki kujaza kuponi za bahati nasibu.
Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.
Akizungumza na wakazi eneo hilo, Ofisa Masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda alisema kuwa zimebaki siku sita hivyo wachangamkie fursa hiyo kwani inaweza kuwa nyumba hiyo mionmghoni mwa wana Tandale.
Katika uhamasishaji huo, Yohana Mkanda alirudia wito wake kwamba: “Siku zimebaki sita nunueni magazeti ya Global mengi na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda nyumba kwani unaweza kuwa wewe au yule na kugeuka baba au mama mwenye nyumba! Hivyo, fursa ndiyo hii, bahati humjia mtu yeyote, kwa hiyo nunua magazeti yetu pendwa yaliyojaa bahati na kila namna kila wakati. Kazi kwako, nyumba ndiyo hiyoo…!!!”
NA DENIS MTIMA/GPL