The House of Favourite Newspapers

Amani latoa zawadi kwa wauza magazeti

0
Afisa usambazaji wa Global Publishers, Jimmy Haroub akimpa zawadi muuza magazeti Richard Daud anayefanyia kazi zake maeneo ya Morocco mpaka Namanga.

Gazeti la Amani ambalo linachapishwa na Global Publishers pamoja na magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Ijumaa, pamoja na Ijumaa Wikenda leo limegawa zawadi ya kiasi cha pesa shilingi 10,000 kwa wauza magazeti ambao wamekuwa wakifanya vizuri kimauzo.

 

Jimmy akimkabidhi muuza magazeti wa mitaa ya Kinondoni Mahakamani aitwaye Msafiri Geofrey.

Amani lilitembelea mitaa ya Morocco jijii Dar na kumpa zawadi Richard Daud, ambapo mitaa ya Kinondoni zawadi ilikwenda kwa Msafiri Geofrey na mitaa ya Temeke- Mwembe Yanga lilimpa zawadi Mohammed Machela.

Jimmy akimkabidhi zawadi ya pesa, Mohammed Machela, muuza magazeti wa Temeke-Mwembe Yanga.

 

Jimmy Haroob akichukua maoni ya msomaji wa gazeti la Amani, mitaa ya Temeke- Mwembe Yanga.

 

Stori: Boniphace Ngumije

Leave A Reply