The House of Favourite Newspapers

Amazon Kuwaachisha Kazi Zaidi ya Watu 18,000 ili Kupunguza Gharama

0

Amazon inalenga kufunga Zaidi ya nafasi 18,000 za kazi ili kupunguza gharama, bosi wa kampuni hiyo kubwa ya teknolojia anasema.

Wafanyakazi walioathirika watajulishwa kuanzia tarehe 18 Januari, Afisa mkuu mtendaji Andy Jassy alisema katika barua kwa wafanyakazi .
Punguzo hilo ni karibu 6% ya wafanyikazi wa kampuni takriban 300,000 .
Amazon ndio kampuni kubwa ya hivi punde ya kiteknolojia kufichua upunguzaji wa wafanyikazi wengi kwani gharama ya juu ya maisha inawafanya wateja kupunguza ununuzi wa bidhaa.
Tangazo hilo linakuja baada ya kampuni hiyo kubwa ya teknolojia kusema mwaka jana kwamba itapunguza idadi ya wafanyakazi wake
“Tunajitahidi kusaidia wale ambao wameathiriwa na tunatoa vifurushi ambavyo ni pamoja na malipo ya kuondokaa, marupurupu ya bima ya afya ya mpito, na usaidizi wa uwekaji kazi wa nje,” Bw Jassy alisema.

“Amazon imekabiliana na na hali ya msukosuko wa kiuchumi hapo awali, na tutaendelea kufanya hivyo,” aliongeza.
Bw Jassy hakutaja mahali ambapo wafanyikazi walioathiriwa wapo lakini alisema kampuni hiyo itawasiliana na mashirika ambayo yanawakilisha wafanyikazi “panapofaa katika bara Ulaya”.
Pia alisema “ufutaji mkubwa wa nafasi ” za kazi utakuwa katika shughuli za Maduka ya Amazon na timu yake ya Watu, Uzoefu, na Teknolojia.

Leave A Reply