The House of Favourite Newspapers

Girl Queens mabingwa Castle Africa 5 aside Bonanza

Baadhi ya Wachezaji wa Girl Queens wakishangilia na Kikombe mara baada baada ya kuibuka mabingwa wa Castle Africa 5s Bonanza lililofanyika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 

TIMU mpira wa miguu ya Wanawake yenye makazi yake Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam wameibuka mabingwa katika Bonanza kubwa la Soka Wanawake lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Viwanja vya Leaders kwa udhamini wa Kampuni ya Bia nchini (TBL) kupitia bia yake ya Castle Lager na hivyo kuzawadiwa Kikombe, Medali za dhahabu, Pesa taslimu shilingi 900,000/=, Caton ya bia ya Castle Lager pamoja na kuwakilisha nchi katika mashindano ya Caslte Africa 5s Wanawake yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.

Girls Queen waliutwaa ubingwa kwa kuongoza kuwa na idadi nyingi ya magoli ambayo ni 12, wakifuatiwa na timu ya Msimbazi Queens magoli 9 ambao walikama nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi 600,000/=

Mshindi wa tatu ni Wema Queens ambao walizawadiwa pesa taslimu shilingi 300,000/=

Akizungumza na wachezaji, waandishi wa habari pamoja na wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwenye Bonanza hilo, Menager mauzo wa TBL, Joseph Nicolous alianza kwa kuwapongeza mabingwa Girl Queens kwa kutwaa ubingwa na kuwaomba zawadi ya walizozawadiwa ikawe ni chachu ya maandalizi mazuri ya kuwakilisha Nchi katika mashindano ya Castle Africa 5s Wanawake yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Nicolous pia aliwapongeza washindi wa pili na tatu kwa ushindi pamoja na timu zote zilizoshiliki Bonanza hilo ambazo ni, Chinga Queens kutoka Kariakoo, Siza Sisters kutoka Kariakaoo, Tabata Queens kutoka Tabata, Dragon kutoka Mwananyamala, Bulyaga kutoka Temeke, Mwangaza Queens kutoka Temeke, Furaha Queens kutoka Gerezani, Umoja Queens kutoka Kidongo Chekundu, MRJ Queens kutoka Mlandizi, Wema Dallas Queens kutoka Mlandizi, Jupita kutoka Buguruni Sukita, Mercury kutoka Msimbazi, La Capilla Kutoka Mbagala na Santiago kutoka Mbagala.

Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania(Tbl), Joseph Nicolous(wa pili kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Girl Queens, Zubeda Mgunda kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa wa Castle Africa 5s Bonanza lililofanyika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.(Katikati) ni Balozi wa Castle Africa 5s Tanzania, Ivo Mapunda.

 

Nae Balozi wa Bia ya Castle Africa 5s Tanzania, Ivo Mapundaaliishukuru Kampuni ya Bia Nchini(TBL) kwa maandalizi na uratibu mzuri wa Bonanza ambao umetupa bingwa na mwakilishi mzuri wa mashindayo ya Castle Africa 5s Wanawake yajayo, naamini Girl Queens ni timu nzuri watatuwakilisha vyema na kuhakikisha ubingwa unabaki Tanzania.

Comments are closed.