The House of Favourite Newspapers

Aomba Kuachiwa: “Hati ya Mashtaka si Yangu”

0


MSHTAKIWA namba tatu katika kesi ya unyang’anyi wakutumia silaha, Daniel Mbura ameiomba mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imuachie huru arudi mtaani akapambane na majukumu ya kujenga taifa kwa kuwa taarifa zote za hati ya mashitaka katika kesi hiyo sio zake.

 

Mbura anashitakiwa pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya pamoja na mshirika mwingine, Sylvester Nyengu.

 

Mbura ameiambia Mahakama Agosti 23 kuwa yeye anaitwa Daniel Laurent Mbura (31), Mkulima, Mdigo, Mkazi wa Shamsi nakwamba hati ya mashitaka imekosea kuanzia majina yake, umri, kabila, shughuri anayofanya na sehemu anayokaa.

 

Katika hati ya Mashtaka ya kesi ya jinai namba 105 ya mwaka huu imemtambulisha yeye kama Daniel Gabriel Mbura (38), Mburu, Mfanyabiashara, mkazi wa Boma Ng’ombe Hai.

 

Mbura amesema kesi hiyo ni ya uongo na imetengenezwa. Hakusema kwa nini imetengenezwa na kwanini awe yeye, lakini ametaka mahakama iitupilie mbali kesi hiyo.

 

Leave A Reply