The House of Favourite Newspapers

Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Elneny

0

Elneny (2)Mohamed Elneny

London, England

Yametimia! Kama ulikuwa ukisikia tetesi kila kona kwamba Klabu ya Soka ya Arsenal ya England ilikuwa mbioni kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji kutoka FC Basel ya Uswisi, Mohamed Elneny, basi jua kwamba hiyo si tetesi tena bali ni ‘cofirmed’.

Elneny (3)Akizungumza na waandishi wa habari mpaka stori hiyo kuifikia Umbeya Umbeyani, kocha Arsene Wenger amesema kuwa dili la mchezaji huyo limekamilika kwa kutoa kitita cha paundi milioni 5 (zaidi ya bilioni 10) na hivyo kuna uwezekano wa kucheza mechi ya Jumapili dhidi ya Stoke City.

Elneny (5)Arsene Wenger

“Tunafurahi kumuona amejiunga na sisi, natumaini atakuwepo katika mechi dhidi ya Stoke City siku ya Jumapili,” alisema Wenger baada ya mechi dhidi ya Liverpool iliyomalizika kwa mabao 3-3

Elneny (1)Alexis Sanchez

Mbali na habari hiyo, pia ile iliyo chini ya kapeti inasema kwamba mchezaji wa timu hiyo, Alexis Sanchez anaweza kuwepo hiyo Jumapili baada ya kukosa mechi kadhaa sababu ya kuwa majeruhi.Elneny (4)

Leave A Reply