The House of Favourite Newspapers

Yanga yaendelea kujifua kwa nguvu

0

YANGA (1)

Wachezaji wa timu ya Yanga wakijiweka sawa katika Uwanja wa Boko Veterani, Boko kabla ya kushuka dimbani Jumapili kucheza na Ndanda katika mchezo wa Ligi Kuu utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar.

YANGA (3)

Mshambuliaji wa Yanga, Paul Nonga (aliye mbele jezi namba 26) akijifua kwa ajili ya kujiweka sawa katika mazoezi ya kikosi hicho.

YANGA (2)

Kipa wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’ mwenye jezi nyeusi akiwaongoza wachezaji wengine wa kikosi hicho kufanya mazoezi ya kukimbia katika mazoezi yaliyofanyika leo Alhamisi katika Uwanja wa Boko Veterani, Boko jijini Dar.

YANGA (4)

Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya akimpigisha pushapu kocha msaidizi wa kikosi hicho, Juma Mwambusi kama moja ya sehemu ya mazoezi.

YANGA (5)

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm (aliyesimama) akisimamia mazoezi hayo.

KIKOSI cha Yanga kinachofundishwa na Mholanzi, Hans van Pluijm leo Alhamisi kimeendelea na mazoezi yake katika Uwanja wa Boko Veterani, Boko kwa ajili ya kuivutia kasi Ndanda ya Mtwara wanaotarajia kuvaana nao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa wikiendi hii katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.

(Picha na Musa Mateja / GPL)

Leave A Reply