The House of Favourite Newspapers

Arthshakti Foundation Na Lions Club Dar es Salaam Sky Walivyotoa Matibabu Bure

0
Miss Sukaina wa Lions Club Dar es Salaam Sky.

Dar es Salaam 28 Mei 2023: Taasisi ya Arthshakti Foundation na Lions Club ya jijini Dar es Salaam zimefanya matendo ya huruma kwa wakazi wa Temeke jijini kwa kuwapelekea kambi ya matibabu na kutoa bure huduma za afya kwa watu wa rika zote.

Katika zoezi hilo Lions Club Dar es Salaam imeshirikiana na madaktari wa Hospitali ya Temeke ambapo kwa waliofanyiwa vipimo na kubainika kuwa na matatizo makubwa zaidi yaliyohitaji rufaa walipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya mkoa wa Afya wa Temeke.

Britesh Meta kutoka Arthshakti Foundation akizungumza kwenye tukio hilo.

Akizungumza kwenye kambi hiyo iliyowekwa Temeke Wailes Miss Sukaina kutoka Lions Club Dar es Salaam Sky amesema taasisi hiyo inaunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha afya za wananchi wake.

Miss Sukaina amesema wao na Arthshakti Foundation wamekuwa na utaratibu wa kutoa huduma za afya bure wakiangalia zaidi kwenye matibabu yasiyoambukiza kama vile, magonjwa ya moyo, presha, mtoto wa jicho, kisukari na mengineyo.

Madaktari wakitoa huduma kwa mmoja wa waliojitokeza kupatiwa huduma hiyo.

Ameendelea kusema kuwa katika kituo hicho cha Temeke Wailes wameweka kambi hiyo wakitoa matibabu kwa kushirikiana na Hospitali ya Temeke ambapo hata kama kuna mgonjwa atakayebainika kuwa na uhitaji wa rufaa atapewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Mkoa wa Afya wa Temeke.

Lion Hamis Martin ambaye ni Mwenyekiti wa Huduma kutoka Lions Dar es Salaam Sky akizungumza na Global Tv kwenye kambi hiyo.

Naye Britesh Meta kutoka Arthshakti Foundation kwa upande wake aliwashukuru wote walijitolea kufanikisha zoezi hilo na waliofika kwenye kambi kupata matibabu ambapo shukrani za pekee zilienda kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Temeke, Lions Club Dar es Salaam Sky, Mazingira Plus na wengine wote waliojitolea.

Baadhi ya waliofanikisha zoezi hilo katika picha ya pamoja.

Kwa upande wake msanii Baby Madaha ambaye ni Mkurugenzi wa Shirika la Voice of Women aliwashauri wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye kambi hiyo ili kujipatia matibabu na kupata ushauri nasaha wa jinsi ya kufuata katika kulinda afya zao.

Msanii Baby Madaha akipewa majibu baada ya kupima afya yake kwenye kambi hiyo.

Baby Madaha amesema kambi nyingine kama hiyo wanatarajia kuifanya tena mwezi Agosti mwaka huu ambapo itakuwa katika wilaya nyingine na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi wasikiapo ilipo kambi hiyo. Alimaliza kusema msanii huyo.

Leave A Reply