The House of Favourite Newspapers

Asha Baraka apunguza wanamuziki Twanga Pepeta

0

asha baraka

Na Imelda Mtema, Risasi Jumamosi

BIG Boss wa The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka amewapunguza wanamuziki sita wa bendi yake ili kubaki na wachache watakaoendana na hali ya uchumi ya sasa.

Akizungumza na gazeti hili, mkurugenzi huyo alisema kuwa amefikia uamuzi huo kwa kuona ni bora kuwa na wanamuziki wachache ambao anaweza kuwalipa vizuri kuliko kuwa na wengi na kushindwa kuwahudumia.

“Nimekuwa kama Magufuli lakini mimi kwangu si kwamba walikuwa na makosa bali gharama za kukodi ukumbi, matangazo na vitu kibao vimepanda bei tumeona bora kubaki na wanamuziki wachache ambao tunaweza kuwahudumia,” alisema Asha huku akiyahifadhi majina ya wanamuziki aliowapunguza.

Leave A Reply