The House of Favourite Newspapers

Asilimia 85 ya Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam Wapata Chanjo, Uviko – 19

0
Mwanahabari na Mjumbe wa kamati tendaji ya Jukwaa la Waandishi wa Habari Tanzania (TEF,) Neville Meena akitoa mada katika mkutano huo.

 

 

DAR ES SALAAM imefikia asilimia 85 ya malengo ya utoaji chanjo kwa wananchi  ambao walilengwa kufikiwa na chanjo hiyo ambayo ni salama na muhimu dhidi ya virusi vya corona.

 

Akizungumza mapema leo na waandishi wa habari, Afisa Afya wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Enezael Ayo wakati wa mkutano wa majadiliano kuhusu chanjo ya corona amesema kuwa ni jukumu la wana habari kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa chanjo hiyo.

Wanahabari wakiwa katika mkutano huo.

 

 

Mkutano huo ambao uliowakutanisha wataalam wa afya na Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC,) chini ya mradi wa ‘Boresha Habari’ unaofadhiliwa na shirika la Internews.

 

Dkt. Enezael amesema kati ya watu milioni 6 (kwa mujibu wa sensa ya 2012,) watu 2,820,821 wenye umri wa kuanzia miaka 18 wanaoishi katika Jiji hilo wamekamilisha chanjo dhidi ya virusi vya UVIKO-19 ambapo zoezi hill lililenga kuwafikia wananchi 3,310,079 mpaka sasa wamefika asilimia 85 mpaka sasa wameendelea kuhamasisha wananchi ili waweze kufikiwa na huduma ya uchanjaji.

Mtaalam wa masuala ya afya Dkt. Christina Mdingi akizungumza katika mkutano huo.

 

 

“Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzindua rasmi zoezi la chanjo Agosti 30 mwaka jana Dar es Salaam tuliweka nguvu katika kuhakikisha wananchi wanapata elimu na kupata chanjo,kipindi tunanza tulikuwa na vituo vitatu  hadi kufikia vituo 318 mpaka kwa sababu wananchi wameelimika na wameona umuhimu wa kupata chanjo.

 

Ameendelea kusema kuwa makundi yaliyopewa kipaumbele katika upataji wa chanjo ya UVIKO-19 ni wazee kuanzia miaka 50 na kuendelea, watoa huduma za afya, wenye magonjwa sugu pamoja na kundi la vijana ambalo huambukiza na kuambukizwa virusi vya uviko 19.

 

‘’Wananchi wanatakiwa kuelimishwa zaidi ili waweze kupata chanjo hii tunashukuru wadau wa maendeleo wakiwemo MDH, Benjamini Mkapa, wanahabari, wahudumu wa afya ngazi ya jamii na wenyeviti wa mitaa kwa uhamasishaji tuendelee kumalizia asilimia zilizobaki ili kufikia lengo.

 

‘’Tulifanya utafiti mdogo kuhusu tahadhari zilizochukuliwa dhidi ya UVIKO 19 kwa kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni magonjwa ya minyoo na ya aina hiyo yamepungua kwa hiyo yukagundua unawaji mikono kwa maji safi tiririka kunaepusha magonjwa mengi hivyo basis tunaendelea kutoa elimu kwa wananch kwa sababu, Dar es Salaam ni jiji la biashara mwingiliano ni mkubwa kupitia kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli na Uwanja wa ndege.’’ Amesema.

 

Nae mtaalam wa masuala ya afya Dkt. Christina Mdingi amesema chanjo ya UVIKO-19 ni salama na muhimu dhidi ya virusi hivyo na kuvitaka vyombo vya habari kusimama katika nafasi yao ya kuelimisha na kutoa taarifa sahihi kwa Umma wa watanzania ili waweze kupata chanjo.

 

“Waandishi wa habari mna uwezo wa kufikisha ujumbe kwa jamii kwa haraka zaidi hivyo basi nendeni mkafikishe ujumbe ili wananchi waanchane na uzushi unaondelea ikiwemo kuwa wanaume wakichanjwa nguvu za kiume hupungua ,kwamba ukichanja unageuka zombi na mengineyo,”Amesema.

 

Pia Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC,) Samson Kamalamo ameishukuru Internews kwa kuratibu mafunzo hayo yaliyogusa sekta ya afya na kuwataka waandishi wa habari kuzingatia weledi pindi wanapoandaa na kuchakata habari kabla ya kuyafikisha kwa jamii kwa kuwa tasnia ina nguvu ya kuaminika.

Leave A Reply