The House of Favourite Newspapers

Maembe Yenye Bei Kubwa Zaidi Duniani Yauzwa Katika Mnada

0
Maembe yakiwa sokoni kwa ajili ya kuuzwa kwa wateja

MAEMBE haya yaitwayo Taiyo na Tamago ama Egg of the Sun ni maembe matamu na yenye sukari asilimia 15 zaidi tofauti na maembe mengine, maembe haya yanahitaji hali ha hewa yenye joto na muda mrefu kuwepo kwenye jua ili kupata utamu wa maembe hayo.

 

Matunda haya hukuzwa nchini Japan, kwenye nyumba ya kioo sababu hali ya hewa inaweza sababisha uharibifu wa mimea hiyo ya maembe.

Maembe maarufu kama Egg of the Sun

Tunda hili hupimwa ubora kwa kutumia vigezo vya ubora vya maembe hayo vilivyowekwa kama vile uzito inabidi kufikia gramu 350 na sukari izidi kwa asilimia 15 tofauti na maembe ya kawaida yalivyo.

 

Kwa kila mwaka maembe yaliyo bora huchaguliwa na kupelekwa kwenye mnada na kuuzwa kwa 448,222.50-yen kwa dazani ambayo ni sawa na 6.996,000.00 kwa pesa za kitanzania, maembe haya yana thamani kubwa kwenye soko la mnada wa Japan na yameweza kujichukulia umaarufu kwa sana.

Maembe haya yamepata umaarufu mkubwa Duniani na yanazalishwa nchini Japan

Kwa mwaka wa 2019 mnada wa maembe ya Miyazaki ulianza saa moja asubuhi na kuleta mzozo kwa umati wa watu baada ya bei yake kutangazwa, maembe hayo yalipelekwa kwenye kampuni ikiwa na uzito wa kilo moja yakiwa yamewekwa kwenye kontena na maembe hayo kuishia kuuzwa kwenye duka la Fukuoka, mji mkubwa huko mkoa wa Kyushu ambapo Miyazaki inapatikana.

Leave A Reply