The House of Favourite Newspapers

Askari Auawa Kwa Risasi Na Askari Mwenzie Kisa Chadaiwa ni Wivu Wa Mapenzi

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo

ASKARI Magereza Faustine Masanja wa Gereza la Kisongo anadaiwa kumuua askari mwenzake aliyefahamika kwa jina la Ombeni Mwakiyani kwa kumpiga risasi kichwani kisa kikidaiwa ni wivu wa mapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Charles Mkumbo akiongea na mtandao wa Global Publishers amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea leo majira ya asubuhi wakati wakiwa kazini kwenye Gereza la Mkoa la Kisongo.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakuwa tayari jina lake liandikwe mtandaoni alidai kuwa, Masanja alimpiga risasi mwenzake wakiwa wanawapakia mahabusu kwenye gari kwa ajili ya kuwapeleka kwenye mahakama mbalimbali kwa ajili ya kusikiliza kesi zao.

Hata hivyo, baadhi ya askari magereza ambao hawakuwa tayari majina yao kuandikwa walidai kuwa Ombeni na Masanja wake zao ni ndugu hivyo kuna uwezekano kulikuwa na mgogoro wa kifamilia.

Comments are closed.