The House of Favourite Newspapers

Askari Polisi Afia Gesti Akijiburudisha na Mrembo

0

JESHI la Polisi nchini Kenya linafanya uchunguzi kufuatia mwanaume mmoja, ambaye ni askari wa Jeshi hilo mwenye umri wa miaka 55 kufariki dunia katika chumba cha hoteli mjini Ndhiwa Kaunti ya Homa Bay nchini humo wakati akijiburudisha na mrembo aliyetoka naye kimahaba.

 

Kamanda wa Polisi Kaunti Ndogo ya Ndhiwa, Paul Rioba amesema kuwa kisa hicho kilitokea usiku wa Ijumaa, Januari 21, ambapo askari huyo ambaye jina lake limehifahdiwa, alipoteza fahamu na kufariki wakati wa kushiriki tendo la ndoa na mrembo huyo mwenye umri wa miaka 25.

 

“Mwanaume huyo alifariki akiwa chumbani na mwanamke huyo. Kwa mujibu wa mwanamke huyo ambaye tunamshikilia, mwanaume huyo alizimia na kuaga dunia wakati wa tendo la ndoa,” Rioba alisema.

 

Mwanaume huyo anasemekana kuwasili wa kwanza na kulipia chumba chao cha hoteli huku mwanamke huyo akijumuika naye baadaye.

 

Katika taarifa aliyotolewa na polisi, mwanamke huyo alisema kuwa mwanaume huyo alipozimia. ilimlazimu kuwaarifu wasimamizi wa hoteli hiyo, ndipo hapo maofisa wa polisi walipoarifiwa kuhusu tukio hilo na mwanamke huyo kutiwa mbaroni.

 

“Ametiwa mbaroni anapoendelea kusaidia polisi katika uchunguzi. Hatutaki kuotea chochote kwa sasa hadi pale ambapo upasuaji wa mwili utafanywa ili tubaini kilichojiri,” Rioba alisema. Mwili wa marehemu ulipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Manyatta Kabodo ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

Leave A Reply